Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Yahaya Omary Massare

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Manyoni Magharibi

Primary Question

MHE. YAHAYA O. MASSARE K.n.y. MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha Zao la Kitunguu linawanufaisha Wananchi wa Mkoa wa Singida?

Supplementary Question 1

MHE. YAHAYA O. MASSARE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Ninaipongeza Serikali kwa majibu mazuri sana ambayo yana manufaa makubwa sana kwa wananchi wa Mkoa wa Singida, lakini nina maswali mawili.

Mheshimiwa Naibu Spika, ipo ahadi ya Mheshimiwa Waziri katika eneo la Njiapanda ya Melia kujenga soko la vitunguu. Je ni lini ahadi hii utaitimiza?

Mheshimiwa Naibu Spika, pia katika Halmashauri ya Itigi tunalima vitunguu. Changamoto maeneo yanayozunguka Itigi yana changamoto ya oevu kipindi cha masika. Je, Serikali sasa ipo tayari kwenda kuyakusanya yale maji na kutengeneza bwawa kuzunguka katika Mji huo wa Itigi ili wananchi walime vitunguu kwa wingi?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu soko alilolitaja, vile vile ilikuwa ni maelekezo ya Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi. Nimhakikishie Mheshimiwa Mbune kwamba ipo kwenye bajeti ya mwaka ujao wa fedha 2025/2026, hilo soko litaanza kujengwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu eneo oevu la Itigi, ninataka na yeye mwenyewe amekuwa akifuatilia sana, wataalam wa Wizara ya Kilimo wameshaanza kufanya usanifu wa maeneo yote ambayo yanatuama maji katika Wilaya ya Bahi na Wilaya ya Manyoni. Kwa hiyo, maeneo yote haya yataingizwa katika mpango wa Serikali ili tuweze kuyafanyia kazi.