Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 33 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 427 2025-05-27

Name

Aysharose Ndogholi Mattembe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. YAHAYA O. MASSARE K.n.y. MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE aliuliza: -

Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha Zao la Kitunguu linawanufaisha Wananchi wa Mkoa wa Singida?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Aysharose Ndogholi Matembe, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuwanufaisha wakulima wa zao la kitunguu….

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri sogeza hiyo mic.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Naam.

NAIBU SPIKA: Iweke mic vizuri.

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ili kuwanufaisha wakulima wa zao la kitunguu katika Mkoa wa Singida na maeneo mengine nchini, Serikali inaendelea kutoa mbolea ya ruzuku, mafunzo ya kanuni za kilimo bora cha vitunguu na kuwapatia Maafisa Ugani vitendea kazi zikiwemo pikipiki na vifaa vya kupima afya ya udongo ili kutoa ushauri sahihi wa matumizi ya mbolea na hivyo kuongeza tija na uzalishaji wa zao hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, vilevile Serikali inaendelea na ujenzi wa skimu za umwagiliaji zenye jumla ya hekta 7,300 katika Kata zinazolima zao la kitunguu za Msange, Masimba na Msingi. Kukamilika kwa ujenzi wa Skimu hizo kutanufaisha wakulima 52,000 wa vitunguu katika vijiji 19 vilivyopo katika Kata za mradi huo.

Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, Serikali katika mwaka 2025/2026 itaanza kujenga masoko kwa ajili ya zao la vitunguu katika Mkoa wa Singida na maeneo mengine nchini pamoja na kuandaa kanuni kwa ajili ya kuzuia ufungashaji wa lumbesa.