Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Jesca Jonathani Msambatavangu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Iringa Mjini

Primary Question

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU aliuliza: - Je, Serikali imefanya tathmini gani ya vinywaji ilivyoruhusu kama pombe kuona kama havina athari kwa wananchi hasa vijana?

Supplementary Question 1

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu hayo, nina maswali mawili ya nyongeza. Swali la kwanza, je, uthibiti huo wa kupata pombe zenye ubora wamepeleka mpaka kwenye pombe zile zinazotengenezwa za kienyeji?

Mheshimiwa Naibu Spika, pili, kuna tathmini yoyote ambayo wameifanya kujua athari ya pombe hasa zile zenye content kubwa ya alcohol namna zinavyosababisha vifo nchini?

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nichukue nafasi hii pia kumpongeza Mheshimiwa Jesca Msambatavangu kwa kufuatilia na hasa kwenye afya na zaidi kwenye watumiaji wa vilevi au vileo ambavyo vinazalishwa katika nchi yetu na vingine vinaendelea kutoka nje ya nchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imekuwa ikifanya kazi kubwa sana. Moja, kuhakikisha kama nilivyosema tunadhibiti ubora wa pombe zinazozalishwa nchini na zile zinazoingia nchini. Kwenye eneo hili la pombe za kienyeji, nikuhakikishie kwamba Serikali tumeshaanza kufanya kazi kubwa moja, kwa kushiriki na taasisi zetu za TBS, SIDO na TILDO, tunafanya utafiti wa pombe za kienyeji ambazo tunaona zinakidhi viwango ili ziingizwe kwenye ubora na kuwasaidia wazalishaji wadogo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, tunavyoongea hivi sasa pombe za kienyeji kama rubisi, pia na ulanzi kule kwetu na pombe nyingine kama za ndizi nakumbuchi ambazo zilikuwa za kienyeji sasa tunazilazimisha kwa kuwapa viwango ili ziweze kuwa na ubora kupunguza athari kwa wanywaji ambao wakati mwingine wanaweza kunywa zaidi kuzidi kiwango kinachotakiwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na tathmini ya athari za pombe ambazo zimekuwa zimezidi au wanazokunywa zaidi ya viwango au zile zenye content ya alcohol kubwa, Serikali kupitia Wizara ya Afya hufanya hivyo na Waziri wa TAMISEMI, lakini na sisi kama Wizara ya Viwanda na Biashara kama nilivyosema, pale tunapobaini kwamba pombe fulani ina kileo kikubwa kuzidi viwango na nyingine kama tulivyosema za kienyeji kama gongo na nyingine huwa tunapiga marufuku, lakini pia kufuatilia ili kudhibiti athari hizi ambazo zinaweza zikatokana na wingi wa kileo katika pombe za kienyeji na za viwandani.

Name

Festo Richard Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makete

Primary Question

MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU aliuliza: - Je, Serikali imefanya tathmini gani ya vinywaji ilivyoruhusu kama pombe kuona kama havina athari kwa wananchi hasa vijana?

Supplementary Question 2

MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, mbali na majibu ya Serikali, ukifuatilia ripoti ya Muhimbili inaonyesha kwamba vijana wengi wamepata tatizo la blood dialysis kutokana na matatizo ya figo na vitu vingine kutokana na pombe feki na pombe ambazo zimezidi content ambazo zinazagaa mtaani. Je, Wizara mbali ya kuzingatia biashara, ina wajibu wa kulinda Taifa kwenye afya ya vijana; Wizara hii haioni kwamba kuwe na mkakati maalum, operation maalum kuondoa vinywaji ambavyo vimekuwa vikiangamiza nguvu kazi ya Taifa letu?

Name

Exaud Silaoneka Kigahe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kaskazini

Answer

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, nichukuwe nafasi hii kumpongeza ndugu yangu Mheshimiwa Festo Sanga kwa swali hili muhimu sana. Ni kweli kama nilivyosema, moja ya changamoto ni hii ya matumizi ya pombe ya kuzidi kiasi na hasa kama alivyosema mfano kwa vijana na kumekuwa na changamoto hizo mbalimbali ikiwemo hiyo ya figo na mambo mengine.

Mheshimiwa Naibu Spika, moja, kama Serikali nimesema tunadhibiti ubora/viwango vya vinywaji hivi/vileo. Pili, pombe zile feki kupitia taasisi zetu ikiwemo TBS, lakini pia Fair Competition Commission huwa tunapita mitaani kusaka kwa kushirikiana na wazalishaji. Kwa mfano, kwenye suala la feki, kweli kumekuwa na pombe baadhi ni feki, mfano konyagi, baadhi ya wazalishaji na ambao sio waadilifu wanachukuwa zile chupa ambazo ni za pombe fulani, wanaweka pombe kali ambazo zina madhara, tumekuwa tukikamata. Tunashirikiana na wazalishaji kuhakikisha tunadhibiti hilo.

Mheshimiwa Naibu Spika, zaidi tunaendelea kutoa elimu kwa watumiaji. Sisi wote tunatumia vileo kuhakikisha tunatumia kwa kiasi, lakini pia kufuata viwango na kujiridhisha kwamba pombe unayokunywa ni ile ambayo ni nzuri na imetoka kwenye wazalishaji halisi badala ya kufuata kwa sababu wengine wanafuata urahisi wa bei…

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa, maliza majibu.

NAIBU WAZIRI WA VIWANDA WA VIWANDA NA BIASHARA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru sana.