Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 33 | Industries and Trade | Wizara ya Viwanda na Biashara | 425 | 2025-05-27 |
Name
Jesca Jonathani Msambatavangu
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Iringa Mjini
Primary Question
MHE. JESCA J. MSAMBATAVANGU aliuliza: -
Je, Serikali imefanya tathmini gani ya vinywaji ilivyoruhusu kama pombe kuona kama havina athari kwa wananchi hasa vijana?
Name
Exaud Silaoneka Kigahe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kaskazini
Answer
NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kupitia Shirika la Viwango Tanzania (TBS) hufanya udhibiti wa bidhaa za pombe kwa kupitia mifumo iliyowekwa ili kuhakikisha ubora na usalama wake. Mifumo ya udhibiti inahusisha uandaaji wa viwango; uthibitishaji ubora wa pombe zinazozalishwa nchini na zinazotoka nje ya nchi; ukaguzi, uchunguzi wa kimaabara; ufuatiliaji katika soko; na kutoa mafunzo na elimu kwa wadau.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali hufanya Tathmini kupitia ufuatiliaji wa bidhaa za pombe na imekuwa ikifanyika mara kwa mara ili kuendelea kubaini na kusimamia ubora wake.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved