Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Nicodemas Henry Maganga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mbogwe
Primary Question
MHE. NICODEMAS H. MAGANGA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa ajira kwa wahitimu wa vyuo nchini?
Supplementary Question 1
MHE. NICODEMAS H. MAGANGA: Mheshimiwa Naibu Spika, ninaanza kwa kuipongeza Serikali, kweli imejenga miundombinu ya elimu, na afya lakini mazingira wanayokaa watumishi hakuna nyumba na makazi. Serikali ina mpango gani wa kuwajengea maeneo ya kuishi ili kusudi hata wanapotoa huduma za kiafya wawe karibu na maeneo?
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, Halmashauri ya Wilaya ya Mbogwe ni mpya, kwa hiyo changamoto bado zipo nyingi sana ambazo zinawakabili watumishi wa Halmashauri hiyo ya Mbogwe. Je, kuna mpango gani wa kuwapiga tough ili na wao waweze kufanya shughuli zao vizuri waweze kuendelea na majukumu yao ya kiutumishi?
Name
Deus Clement Sangu
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kwela
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, nimpongeze Mheshimiwa Maganga, amekuwa mstari wa mbele kuja pale Ofisi ya Rais, Utumishi kufuatilia masuala ya watumishi wa Jimbo lake la Mbogwe. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, nikijibu maswali yake yote mawili kwa pamoja juu ya mazingira ya makazi ya watumishi wa Mbogwe, na ukizingatia na halmashauri mpya, kwanza, nichukue fursa hii kumshukuru sana Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa dhamira yake ya dhati ya kujali maslahi ya watumishi wa umma. Amefanya hivyo siyo tu kuboresha maslahi na kuwapandisha madaraja, hata kujali suala la kujenga makazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, katika halmashauri mpya 39 amejenga nyumba za Wakurugenzi, Wakuu wa Idara nyumba 58 wamejengewa, lakini nyumba za walimu zipatazo 1,700 zimejengwa, na wataalamu wa kada ya afya pia wamejengewa takribani nyumba 270. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimtoe shaka Mheshimiwa Maganga, katika bajeti iliyopitishwa na Ofisi ya Rais, TAMISEMI hapa, pia kuna bajeti ya kujenga nyumba kama zilivyojengwa katika kipindi cha mwaka wa fedha uliopita. Kwa hiyo, nimhakikishie kwamba hili jambo litakuja kufanyika kwenye jimbo lake kwa kuwa pia ni sehemu ambayo tutaipa kipaumbele. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved