Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 33 Public Service Management Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora) 422 2025-05-22

Name

Nicodemas Henry Maganga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mbogwe

Primary Question

MHE. NICODEMAS H. MAGANGA aliuliza:-

Je, Serikali ina mpango gani wa kutoa ajira kwa wahitimu wa vyuo nchini?

Name

Deus Clement Sangu

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kwela

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu:-

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2023/2024, Serikali imetoa nafasi 47,404 za ajira mpya kwa kada mbalimbali ambazo utekelezaji wake unaendelea kupitia Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma na mamlaka nyingine na wasailiwa kutoka vyuo mbalimbali waliofaulu wameweza wamepangiwa vituo vya kazi.

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali inatarajia kutoa ajira mpya 45,000 kwa kada mbalimbali ambazo utekelezaji wake utafanyika kabla ya mwaka huu wa fedha kwisha. Aidha, katika mwaka wa fedha 2025/2026 Serikali imeidhinisha jumla ya nafasi 41,500 za ajira mpya kwa kada mbalimbali ili kuweza kuajiri wahitimu stahiki. Ninashukuru.