Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Agnes Elias Hokororo
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. AGNES E. HOKORORO K.n.y. MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA aliuliza:- Je, lini Vituo vya Afya Kitaya na Majengo - Nanyamba vitapatiwa magari ya kubeba wagonjwa?
Supplementary Question 1
MHE. AGNES E. HOKORORO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza niweke Kumbukumbu za Bunge sahihi, ni Halmashauri ya Wilaya ya Nanyamba siyo Nanyumbu. Nanyumbu ni Halmashauri nyingine. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya masahihisho hayo, sisi wananchi wa Nanyamba tunamshukuru sana Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupata gari katika Kituo cha Afya cha Majengo, lakini nina maswali mawili madogo ya nyongeza. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa Naibu Waziri Kituo cha Afya cha Kitaya kipo mpakani kabisa mwa Tanzania na Msumbiji na hayo maeneo ninadhani unayafahamu. Je, Serikali ina mkakati gani wa haraka wa kutupatia gari ya wagonjwa katika kituo hicho? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili. Halmashauri ya Wilaya Nanyamba kwenye hospitali ile ya halmashauri na hivyo vituo vya afya tuna x-ray machine mbili, lakini katika hizo x-Ray machine mbili zote hatuna mtaalamu hata mmoja, hivyo kuwasababishia wananchi kwenda umbali mrefu kupata huduma ya x-ray.
Mheshimiwa Naibu Spika, je, Serikali ina mkakati gani wa haraka kutupatia wataalamu ambao tumewaomba kwa muda mrefu ili wananchi wakapate huduma hiyo ya x-ray badala ya kusafiri umbali wa kilometa 100 ama 150? (Makofi)
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Agnes Hokororo aliyeuliza swali hili kwa niaba na ninaomba nimtaarifu kwamba Serikali ya Awamu ya Sita tayari imenunua magari ya kubebea wagonjwa 382, lakini imenunua magari 210, kwa ajili ya uratibu ambapo magari haya yamesambazwa kote nchini, lakini ikiwemo Halmashauri ya Wilaya ya Nanyamba. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, ninafahamu uhitaji mkubwa ambao Kituo cha Afya cha Kitaya inao na hasa katika kupata gari la wagonjwa, lakini ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali kama vile ilivyoanza kutangulia kununua magari haya ya kubebea wagonjwa 382, itanunua magari mengine na kuyasambaza katika maeneo yenye uhitaji mkubwa ikiwemo katika Kituo hiki cha Afya cha Kitaya. (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusiana na swali lake la pili kuhusu mtaalamu wa x-ray machine, Mheshimiwa Abdallah Dadi Chikota, alifika katika Ofisi zetu na akawa ameeleza uhitaji huu mahususi kabisa, na ninaomba nimhakikishie kwamba tayari suala hili tunalifanyia kazi ili waweze wapatikane hawa watumishi wataalamu wa mashine hizi za x-ray ambazo zitawasaidia wananchi kupata huduma bora za afya. Tutaleta wataalamu ili waweze ku-operate machine hizi na kuweza kutoa huduma bora kwa Watanzania. (Makofi)
Name
Anatropia Lwehikila Theonest
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. AGNES E. HOKORORO K.n.y. MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA aliuliza:- Je, lini Vituo vya Afya Kitaya na Majengo - Nanyamba vitapatiwa magari ya kubeba wagonjwa?
Supplementary Question 2
MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakushukuru. Wilaya ya Kyerwa kijiografia ni pana sana na tuna vituo vya afya vitano, tukiwa na magari ya wagonjwa wawili Kata ya Murongo pia na Nkwenda. Ni kwa nini sasa Serikali isione umuhimu wa kuweka gari la wagonjwa katika kila tarafa yaani gari iongezeke katika Tarafa ya Mabira ili kurahisisha huduma ya wananchi wetu ambao eneo kijiografia siyo zuri?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, ninaomba nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Mbunge na ninaomba nimpe taarifa kwamba Serikali ya Awamu ya Sita tayari imenunua magari ya kubebea wagonjwa 382 na magari ya uratibu 210.
Mheshimiwa Naibu Spika, dhamira ya Serikali ni kuendelea kununua magari haya na kuyasambaza kote nchini kwa kuzingatia maeneo yenye uhitaji mkubwa. Ninaelewa kwamba katika Wilaya ya Kyerwa, kuna uhitaji mkubwa wa kupata magari haya ya kubebea wagonjwa na ninaomba nikuhakikishie kwamba Serikali italeta magari haya itatafuta fedha, itanunua magari haya, itayasambaza kote nchini ikiwemo Kyerwa kwa ajili ya kutoa huduma bora ya afya kwa Watanzania. (Makofi)
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved