Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 33 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 420 | 2025-05-27 |
Name
Abdallah Dadi Chikota
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nanyamba
Primary Question
MHE. AGNES E. HOKORORO K.n.y. MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA aliuliza:-
Je, lini Vituo vya Afya Kitaya na Majengo - Nanyamba vitapatiwa magari ya kubeba wagonjwa?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Wilaya na Nanyumbu mwaka 2023/2024 imepokea magari mawili ya kubebea wagonjwa ambayo yamepelekwa kwenye Kituo vya Afya Majengo na Hospitali ya Mji wa Nanyamba. Aidha, Kituo cha Afya Kitaya kinahudumiwa na gari kutoka Hospitali ya Mji Nanyamba, ambapo umbali kati ya vituo hivyo ni takribani kilometa 50.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kutenga bajeti kwa ajili ya ununuzi wa magari ya wagonjwa kwa awamu kwa ajili ya vituo vya afya vyenye uhitaji kote nchini kikiwemo Kituo cha Afya Kitaya.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved