Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Rashid Abdallah Shangazi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlalo

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. HUSNA J. SEKIBOKO aliuliza: - Je, kipi chanzo mahsusi cha fedha za kugharamia huduma ya afya kwa mama mjamzito na mtoto chini ya miaka mitano?

Supplementary Question 1

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu ya Serikali, lakini nina swali la nyongeza Kwa kuwa Serikali kupitia Sera ya Afya ina utaratibu wa kuanzisha mifuko mahsusi kwa ajili ya kusaidia hasa katika haya maeneo ambayo yana uhitaji mkubwa, kwa mfano hili la mama mjamzito pamoja na watoto chini ya miaka mitano, Serikali haioni sasa kuna umuhimu ikaleta utaratibu wa kutengeneza mfuko mahsusi ambao utabeba jukumu hili? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Shangazi kwa swali lake hili la msingi hasa kwenye hili eneo ambalo kidogo utekelezaji wake unahitaji umakini wa hali ya juu. Wazo lake tunalichukua na kwenda kulifanyia kazi kama ambavyo amelipendekeza, tuone ni namna gani tunaweza tukashirikiana na wadau mbalimbali na kuunda huo mfumo.

Name

Pauline Philipo Gekul

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Babati Mjini

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. HUSNA J. SEKIBOKO aliuliza: - Je, kipi chanzo mahsusi cha fedha za kugharamia huduma ya afya kwa mama mjamzito na mtoto chini ya miaka mitano?

Supplementary Question 2

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa nafasi. Mheshimiwa Naibu Waziri, ni vifaatiba vipi au dawa zipi mama mjamzito anayejifungua kwa operation anapaswa kulipia, kwa maana sasa wanachajiwa? Ni zipi hasa ambazo wanapaswa kulipia? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kulingana na Sera ya Afya hakuna mama mjamzito anayetakiwa kupata huduma zote bure, lakini kama ambavyo nimekwishasema hapa Bungeni kwa sababu ya changamoto mbalimbali, imewezekana kuwalipia bure 65% ya akina mama, lakini 35% wamekuwa wakipata changamoto mbalimbali kutokana na masuala ya kibajeti, lakini pia na uzembe wa utendaji katika maeneo husika.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nadhani siyo kwamba ni la kusema specific hiki na hiki kinatakiwa kilipiwe, na hiki hakitakiwi kulipiwa. Mama mjamzito kulingana na sera, anatakiwa kupata huduma. Tukishirikiana na hospitali zetu pamoja na Serikali za maeneo husika kwa maana ya wilaya husika au mkoa husika, tunaweza tukapunguza hili tatizo kwa pamoja.

Name

Salma Rashid Kikwete

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Mchinga

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI K.n.y. MHE. HUSNA J. SEKIBOKO aliuliza: - Je, kipi chanzo mahsusi cha fedha za kugharamia huduma ya afya kwa mama mjamzito na mtoto chini ya miaka mitano?

Supplementary Question 3

MHE. SALMA R. KIKWETE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Huduma ya afya kwa mama mjamzito na watoto ni jambo muhimu na la msingi katika kunusuru changamoto zinazojitokeza kwa watoto hawa na mama yao. Sasa, je, ni lini Serikali itatupatia fedha ili kuweza kujenga Kituo cha Afya kule Nangaru, ili mama mjamzito na watoto hawa waweze kupata huduma hizo? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Mbunge mama yetu Salma Kikwete, moja kwa kazi kubwa sana wakati akiwa First Lady aliyoifanya kwenye eneo la mtoto wa kike, amefanya kazi kubwa sana. Pia kwa kazi kubwa anayoendelea kuifanya kwenye jimbo lake. Nimwambie tu, nikitoka hapo tutafanya mawasiliano na DMO wake na uongozi wa wilaya ili tuweze kujua wameweka nini kwenye mpango kwa kushirikiana pamoja na TAMISEMI tuweke huu mkakati wa pamoja wa kuhakikisha hicho kituo kinaenda kujengwa na bajeti ya mwaka ujao.