Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Antipas Zeno Mgungusi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Malinyi
Primary Question
MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI aliuliza: - Je, lini Serikali Itapeleka Magari kwa Jeshi la Polisi Malinyi ili liweze Kutoa Huduma Stahiki kwa Wananchi?
Supplementary Question 1
MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa majibu ya Serikali, lakini kwa ukubwa wa Wilaya ya Malinyi, huhitaji walau magari matatu kwa uchache sana lakini magari mawili ambayo Mheshimiwa Waziri ameyataja moja halipo kwenye hali nzuri. Je, Serikali iko tayari kutuongezea gari muda wowote mwaka huu? Hilo la kwanza.
Mheshimiwa Naibu Spika, la pili ni shukurani kwa Mheshimiwa Waziri na Kamanda IGP kwa kutupatia fedha kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Polisi kwa maana cha OCD katika eneo la Kipingo. Ahsante sana, nasubiri majibu ya swali la kwanza.
Name
Innocent Lugha Bashungwa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Karagwe
Answer
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nampongeza Mheshimiwa Antipas Mgungusi kwa jitihada nzuri anazozifanya za maendeleo kwa ajili ya Jimbo lake la Malinyi, lakini pamoja na jitihada hizi amekuwa akifuatilia masuala ya vitendea kazi kwa upande wa Jeshi la Polisi jimboni kwake.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu swali lake la gari lingine kwa ajili ya kuimarisha usalama kule Malinyi, naomba nimwahidi Mheshimiwa Antipas, kwamba tutaongeza gari lingine la OCCID kwenye miezi ijayo ili kwenda kuimarisha ulinzi kwenye jimbo lake.
Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nitumie nafasi hii kuwaambia Waheshimiwa Wabunge, kuna magari ya OCCID (Wapelelezi wa Wilaya), kwamba kufikia mwezi Agosti, Mungu akijaalia tunapanga kuyasambaza nchi nzima kila wilaya ili kuimarisha ulinzi na usalama.
Mheshimiwa Naibu Spika, natumia nafasi hii kuwahakikishia Watanzania kuwa tumejipanga ipasavyo kuhakikisha uchaguzi wa mwaka huu unafanyika kwa amani na usalama, na tumejipanga kwenye vitendea kazi pamoja na utimamu wa Jeshi la Polisi na vyombo vingine kuhakikisha kila atakayepanga kufanya fujo anashughulikiwa kwa mujibu wa sheria. (Makofi)
Name
Athumani Almas Maige
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tabora Kaskazini
Primary Question
MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI aliuliza: - Je, lini Serikali Itapeleka Magari kwa Jeshi la Polisi Malinyi ili liweze Kutoa Huduma Stahiki kwa Wananchi?
Supplementary Question 2
MHE. ATHUMAN A. MAIGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana. Namwuliza Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani, katika Kijiji cha Ishihimulwa Kata ya Bukumbi, Mbunge na wananchi tumejenga kituo kizuri na cha kisasa lakini hatuna usafiri. Tunaomba atufikirie gari au pikipiki. (Makofi)
Name
Innocent Lugha Bashungwa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Karagwe
Answer
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, kama ambavyo nimesema kwanza, kwa Wilaya za Kipolisi ambazo zilikuwa hazijapata magari awamu ya kwanza, hivi sasa tayari tumeshapeleka magari mapya, Land Cruiser kwenye Wilaya zote za Kipolisi ikiwemo Wilaya za Mkoa wa Tabora.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kama gari halijafika, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Almas, mpango huu kama mlikuwa hamjapata gari ile awamu ya kwanza; awamu ya pili tumeshapeleka magari, nita-check kama halijafika basi nihakikishe linafika. Vilevile, hata kwenye mpango wa OCCID nchi nzima kupata magari Land Cruiser mapya kufika Agosti, pia na hili tutalizingatia. (Makofi)
Name
Hussein Nassor Amar
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nyang'hwale
Primary Question
MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI aliuliza: - Je, lini Serikali Itapeleka Magari kwa Jeshi la Polisi Malinyi ili liweze Kutoa Huduma Stahiki kwa Wananchi?
Supplementary Question 3
MHE. HUSSEIN N. AMAR: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Wilaya ya Nyang’hwale pamekuwa na mwingiliano wa watu wengi kwa ajili ya kuja kuchimba madini na tuna Ofisi ya Uhamiaji pale na wako wawili hawana hata gari, je, Serikali iko tayari kutuongezea Watumishi wa Uhamiaji pamoja na kutupatia gari la ofisi? (Makofi)
Name
Innocent Lugha Bashungwa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Karagwe
Answer
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze Mheshimiwa Amar, kwa ufuatiliaji. Nimhakikishie, hivi ninavyozungumza, Chuo cha Idara ya Uhamiaji tuna vijana ambao wako kwenye mafunzo. Watakapotoka tutahakikisha tunapeleka Maafisa kwa ajili ya kuimarisha huduma za Idara ya Uhamiaji kule Nyang’hwale.
Name
Kunti Yusuph Majala
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI aliuliza: - Je, lini Serikali Itapeleka Magari kwa Jeshi la Polisi Malinyi ili liweze Kutoa Huduma Stahiki kwa Wananchi?
Supplementary Question 4
MHE. KUNTI Y. MAJALA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kituo cha Polisi Wilaya ya Chemba kinakabiliana na changamoto kubwa ya samani za ofisi. Kituo kimekamilika, kina zaidi ya miezi nane, lakini wanashindwa kuhamia kwa sababu tu ya ukosefu wa samani za ofisi. Serikali ina mkakati gani wa dharura wa kuwapatia Polisi wetu samani za ofisi ili waweze kulitumia lile jengo lao jipya? (Makofi)
Name
Innocent Lugha Bashungwa
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Karagwe
Answer
WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Naibu Spika, nimesikia hoja ya Mheshimiwa Kunti, ninaomba niichukue tutaifanyia kazi.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved