Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 29 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 374 2025-05-21

Name

Antipas Zeno Mngungusi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Malinyi

Primary Question

MHE. ANTIPAS Z. MGUNGUSI aliuliza: -

Je, lini Serikali Itapeleka Magari kwa Jeshi la Polisi Malinyi ili liweze Kutoa Huduma Stahiki kwa Wananchi?

Name

Innocent Lugha Bashungwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Karagwe

Answer

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, mwezi Septemba, mwaka 2023 Serikali kupitia Jeshi la Polisi iligawa gari moja jipya lenye namba za usajili PT 4851 Toyota Land Cruiser Pickup kwa Wilaya ya Malinyi, hivyo, kufanya wilaya hiyo kuwa na magari mawili ya Polisi yanayofanya kazi. Serikali inaendelea kutenga fedha kutoka kwenye bajeti yake kila mwaka wa fedha kwa ajili ya ununuzi vitendea kazi mbalimbali yakiwemo magari na kuyagawa kwenye mikoa na wilaya zote hapa nchini.