Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Selemani Jumanne Zedi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Bukene
Primary Question
MHE. SELEMANI J. ZEDI aliuliza: - Je, kwa nini Kampuni za CCECC na YAPI MARKEZI zinazojenga SGR Bukene zinatoa ajira zisizohitaji ujuzi kwa Vijana wanaotoka nje ya Bukene? (Makofi)
Supplementary Question 1
MHE. SELEMANI J. ZEDI: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu ya Naibu Waziri, nina maswali ya nyongeza.
Mheshimiwa Naibu Spika, hali ilivyo sasa hivi, Kampuni za CCECC na YAPI MARKEZI ambazo zinajenga Reli ya SGR na wana kambi pale Bukene, wana jumla ya vibarua (wafanyakazi wasio na ujuzi) kama 300; lakini kati ya hawa 300, wanaotoka katika Jimbo la Bukene hawazidi 12. Je, Mheshimiwa Naibu Waziri yuko tayari kuongozana nami ili twende kwenye kambi hii ili akahakiki ukweli?
Mheshimiwa Naibu Spika, ukweli ulivyo ni kwamba, hawa CCECC pamoja na YAPI MARKEZI hata kwa kazi za vibarua wanaleta vijana kutoka Morogoro na Dar es Salaam na vijana wa eneo la pale wanakosa ajira.
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, namshukuru Mheshimiwa Zedi kwa jinsi anavyofuatilia Vijana wa Bukene waweze kupata ajira katika mradi ambao kimsingi unapita katika eneo ambalo yeye ni mwakilishi.
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kumhakikishia Mheshimiwa Zedi kwamba ni maelekezo ya Serikali, wakandarasi mbalimbali wanaotekeleza miradi mbalimbali katika maeneo mbalimbali katika nchi yetu, wahakikishe kwamba wanatoa kipaumbele kwa vijana wa eneo husika hususan wanapokuwa wanatekeleza miradi mbalimbali.
Mheshimiwa Naibu Spika, inaielekeza TRC iende katika eneo husika ikatazame, kama, ambavyo Mheshimiwa Mbunge amekuwa akizungumza, kwamba kuna watu wengi wametoka eneo lile.
Mheshimiwa Naibu Spika, pili, baada ya Bunge hili pengine tutapanga mimi na yeye twende tukajiridhishe; na ninawataka wakandarasi hao sasa waendelee kuhakikisha kwamba wanachukua vijana katika maeneo ambayo miradi hiyo inapita.
Name
Hawa Subira Mwaifunga
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. SELEMANI J. ZEDI aliuliza: - Je, kwa nini Kampuni za CCECC na YAPI MARKEZI zinazojenga SGR Bukene zinatoa ajira zisizohitaji ujuzi kwa Vijana wanaotoka nje ya Bukene? (Makofi)
Supplementary Question 2
MHE. HAWA S. MWAIFUNGA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Changamoto ya vijana wa maeneo husika katika mradi huu siyo Bukene peke yake, hata katika Jimbo la Tabora Mjini, vijana wengi wanaoletwa pale hawatoki Tabora Mjini, wanakuja kutoka mikoa mingine mbalimbali. Nini changamoto hiyo ambayo hata vijana wetu wanaweza kufanya hizo shughuli ambazo wengine wanakuja kutoka mikoa mingine?
Name
David Mwakiposa Kihenzile
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Mufindi Kusini
Answer
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ukisoma takwimu za jumla ya ajira zote katika mradi wetu huu wa SGR kutoka Dar es Salaam mpaka Tabora kwenda mpaka Mwanza na kwenda mpaka Kigoma, tuna vijana au watu walioajiriwa takribani 1,730 na ajira za kati ni 5,659 wakati ajira za chini ni 5,694. Hawa wa ajira za chini wote kwa sehemu kubwa wanatoka nchini mwetu sehemu tofauti tofauti.
Mheshimiwa Naibu Spika, hivyo basi, ninawaelekeza wakandarasi hao kuhakikisha kuwa wanapokuwa wanachagua vijana hao wa ajira za chini wahakikishe kwamba wanatoa msukumo zaidi au kipaumbele zaidi kwenye eneo ambalo mradi huo unapita.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved