Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Cecilia Daniel Paresso
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza: - Je, lini Serikali italipa fidia na riba kwa wananchi wa Manyara Kibaoni Wilayani Karatu waliopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege Manyara?
Supplementary Question 1
MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Naibu Spika nakushukuru. Naomba kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza: -
(a) Je, Serikali sasa ipo tayari kwenda eneo husika kuwapa wananchi hao majibu haya? (Makofi)
(b) Je, ni lini sasa ujenzi wa uwanja huo kwa maana ya upanuzi utaanza rasmi kwa sababu ni muda mrefu pamekuwa kimya na hakuna kinachoendelea?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Naibu Spika, tuko tayari, lakini nina uhakika wananchi watakuwa bado wanatusikiliza kuhusu majibu haya, lakini kama Serikali kwenda pale, tutakwenda kwa ajili ya kuwajulisha namna ya kulipa hiyo riba ya fidia.
Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu ni lini tutaanza, ninataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, mradi huu upo kwenye mpango ambao tunasaidiana na wenzetu wa World Bank. Mkandarasi ameshapatikana, taratibu ziko tayari na tunategemea kickoff. Kumkabidhi mkandarasi haitachukua muda mrefu kwa sababu ni taratibu tu zile za kibenki. Mkandarasi akiwa tayari kukamilisha taratibu zake, basi ujenzi wa uwanja huo utaanza. (Makofi)
Name
Tecla Mohamedi Ungele
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza: - Je, lini Serikali italipa fidia na riba kwa wananchi wa Manyara Kibaoni Wilayani Karatu waliopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege Manyara?
Supplementary Question 2
MHE. TECLA M. UNGELE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Je, ni lini Serikali itawalipa fidia Wananchi wa Nachingwea waliopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Nachingwea?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nitumie nafasi hii tu kuwajulisha Waheshimiwa Wabunge kwamba, sasa hivi viwanja vingi ambavyo hasa tunatumia fedha ya Serikali kwa 100% ujenzi wake umehamia kwenye Wizara ya Uchukuzi chini ya Mamlaka ya Viwanja vya Ndege, ikiwa ni pamoja na hiki Kiwanja cha Nachingwea.
Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, namshukuru Mheshimiwa Mbunge. Ni kwamba, tutawasiliana na wenzetu wa uchukuzi ambao sasa hivi ndiyo uwanja huu uko chini yao tuone Serikali tumefikia wapi kuwalipa wananchi hao fidia.
Name
Dr. Christina Christopher Mnzava
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza: - Je, lini Serikali italipa fidia na riba kwa wananchi wa Manyara Kibaoni Wilayani Karatu waliopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege Manyara?
Supplementary Question 3
MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Naibu Spika, Kiwanja cha Ndege cha Ibadakuli kilichopo Shinyanga kiko karibuni kukamilika, lakini kuna baadhi ya wananchi walitoa maeneo yao ili kuongeza eneo. Je, ni lini waliobaki watalipwa fidia?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kiwanja hicho alichokitaja cha Shinyanga kipo, kinaendelea. Tunamhakikishia Mheshimiwa Mbunge, kama Wizara ya Ujenzi tulishapeleka mahitaji yale ya fedha ambayo ilikuwa imebaki kwa wenzetu wa Hazina na wanalifanyia kazi. Mara watakapokabidhiwa fedha, tutawalipa hawa wananchi ambao wamepisha mradi huo wa uwanja wa ndege, ahsante.
Name
Janejelly Ntate James
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza: - Je, lini Serikali italipa fidia na riba kwa wananchi wa Manyara Kibaoni Wilayani Karatu waliopisha upanuzi wa Uwanja wa Ndege Manyara?
Supplementary Question 4
MHE. JANEJELLY J. NTATE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Napenda kujua, wananchi wa Rangi Tatu, Chamazi, Msongola na Mbande waliowekewa X na wakazuiwa kufanya maendeleo, ni lini watalipwa fidia ili wapishe ujenzi wa barabara?
Name
Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Ileje
Answer
NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye sheria zetu za barabara baada ya kuongeza zile mita 60 tuliweka X ambazo tunatafuta fedha, lakini kama kuna wananchi ambao walikuwa ndani ya mita 45 kwa mujibu wa sheria yetu, maana yake walikuwa wako kwenye reserved. Itategemea, kama ni X nyekundu maana yake hayo wataondolewa bila fidia, lakini X ya kijani maana yake tumeshafanya tathmini na watatakiwa kulipwa fidia yao.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved