Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Kavejuru Eliadory Felix

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buhigwe

Primary Question

MHE. KAVEJURU E. FELIX K.n.y. MHE. SYLVIA F. SIGULA aliuliza: - Je, lini Serikali itatokomeza uvuvi haramu katika Ziwa Tanganyika? (Makofi)

Supplementary Question 1

MHE. KAVEJURU E. FELIX: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.

Swali la kwanza, Serikali ina mikakati gani ya kuzuia nyavu haramu zinazoingizwa nchini kutoka nje ya nchi?

Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, uvuvi endelevu ni pamoja na uvuvi wa vizimba. Serikali ina mipango gani ya kupeleka vizimba katika ziwa Tanganyika?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Jambo moja ambalo nimwambie tu Mheshimiwa Mbunge na awe na uhakika, Serikali inakataza matumizi ya nyavu ambazo hazikubaliki ambazo ziko chini ya kile kiwango ambacho kinatakiwa. Moja ya mikakati tuliyonayo sasa hivi ni kwamba nyavu zote haramu zikitoka nje ya nchi haziruhusiwi kupita katika bandari zetu ama mipaka yetu hapa nchini.

Mheshimiwa Naibu Spika, pia, wale wote wanaohusika na biashara hiyo, endapo wakikamatwa cha kwanza wanafutiwa leseni, zile nyavu zinataifishwa na kuchomwa. Vilevile, tunafuatilia mpaka kule ambako wamekuwa wakichukulia. Wizara imekuwa ikisisitiza sasa, nyavu zianze kutengenezwa hapa nchini kwa kutumia viwanda vya ndani kwa kufuata ile miongozo na taratibu ambazo zinawekwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu vizimba, Ziwa Tanganyika ni miongoni mwa maziwa ambayo yapo katika mikakati ambayo Wizara ya Mifugo na Uvuvi imeiweka, kwamba, kuna vizimba ambavyo tayari vitaletwa kwa ajili ya Ziwa Tanganyika kama ambavyo imefanyika katika Ziwa Victoria. Kwa hiyo, hilo lipo kwenye mipango ya Serikali. (Makofi)

Name

Anatropia Lwehikila Theonest

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. KAVEJURU E. FELIX K.n.y. MHE. SYLVIA F. SIGULA aliuliza: - Je, lini Serikali itatokomeza uvuvi haramu katika Ziwa Tanganyika? (Makofi)

Supplementary Question 2

MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Ukienda katika Wilaya ya Karagwe na Kyerwa na hasa Kata za Kitwechenkura na Songambele utakutana na watu wengi ambao wamekatwa mikono wakisingiziwa kwamba wamevua samaki upande wa Rwanda kwenye Mto Kagere na pia Mto Kafunzo. Nataka nijue utaratibu ambao Serikali inaweza kuweka kwa ajili ya kuongea na Serikali ya Rwanda na kuwaelewesha wavuvi ili waweze kujua mipaka yao, wasivuke kwenye maji ya Rwanda na wakaishia kupata hizi adha ambazo wamekuwa wanazipata miaka yote.

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Mheshimiwa Naibu Spika, nalifahamu, nimekuwa kule. Jambo moja ambalo nimthibitishie tu Mheshimiwa Mbunge, ni kwamba kwanza, kuna mahusiano kati ya hizi nchi wanachama wa Afrika Mashariki, na kuna ile taasisi yetu ambayo inahusika inayoitwa Lake Victoria Foundation kwa ajili ya nchi zote za EAC. Moja ya makubaliano tuliyokuwa tumeingia ni pamoja na kulinda wavuvi kutoka katika nchi wanachama, kwa maana ya Rwanda, Congo pamoja na Tanzania. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, sasa yanapotokea matatizo kama hayo, moja ya kazi ya Wizara ni kuhakikisha kuwa tunafikisha elimu, na pia tuna-report juu ya matukio hayo maovu. Vilevile, Wizara ikishirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani na Jeshi la Ulinzi wa Taifa, imekuwa na hiyo kazi mojawapo ya kuhakikisha usalama unapatikana katika maeneo hayo. Kwa hiyo, sisi tutaongeza kasi ili matendo haya yasiendelee kutokea. Ahsante.