Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 29 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Waziri wa Mifugo na Uvuvi | 371 | 2025-05-21 |
Name
Sylivia Francis Sigula
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. KAVEJURU E. FELIX K.n.y. MHE. SYLVIA F. SIGULA aliuliza: -
Je, lini Serikali itatokomeza uvuvi haramu katika Ziwa Tanganyika? (Makofi)
Name
Dr. Ashatu Kachwamba Kijaji
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Kondoa
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO K.n.y. WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Wizara ya Mifugo na Uvuvi imekuwa ikishirikiana na wadau mbalimbali ikiwemo TAMISEMI ili kuhakikisha rasilimali za uvuvi zinalindwa na kuvunwa kwa njia endelevu. Aidha, Wizara imeendelea kuimarisha vituo vyote vya ulinzi na usimamizi wa rasilimali za uvuvi vilivyopo katika ukanda wa Ziwa Tanganyika kwa kuvipatia vitendea kazi.
Mheshimiwa Naibu Spika, sambamba na hatua hiyo, Wizara imeendelea na mikakati ya matumizi ya teknolojia ya kisasa ya ndege nyuki katika kukabiliana na vitendo vya uvuvi haramu. Aidha, Wizara kwa kushirikiana na asasi zisizokuwa za kiserikali inaendelea kutoa elimu kwa jamii za wavuvi na wadau wengine juu ya athari za uvuvi haramu.
Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kutoa wito kwa halmashauri kuendelea kushirikiana na Wizara katika kudhibiti vitendo vya uvuvi haramu. Pia, natoa wito kwa wavuvi wote nchini, wakiwemo wavuvi wa Ziwa Tanganyika kufanya shughuli zao kwa kuzingatia miongozo, taratibu, sheria na kanuni za uvuvi. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumetokomeza uvuvi haramu hapa nchini ikiwemo Ziwa Tanganyika.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved