Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Charles John Mwijage

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muleba Kaskazini

Primary Question

MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO K.n.y. MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE aliuliza: - Je, nini mawanda ya Mradi wa Bonde la Mto Ngono lililofanyiwa upembuzi yakinifu ili liweze kuendelezwa na lini ujenzi wa Mradi huo utaanza?

Supplementary Question 1

MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO K.n.y. MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali. Tumekuwa tukianzisha miradi kama hii na wananchi wa maeneo hayo wakiondolewa: -

(a) Je, mradi huo utahakikisha kwamba wananchi wa maeneo hayo wanakuwa sehemu ya huo mradi?

(b) Je, Serikali imezingatia kuwa Mkoa wa Kagera kuna uzalishaji mzuri wa kahawa, kwamba kwenye huu mradi na zao la kahawa litazingatiwa na kupewa kipaumbele ili kuongeza tija na kuongeza uzalishaji wa zao la kahawa?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Nimthibitishie tu Mheshimiwa Kikoyo kwamba, maeneo yote ambayo tunajenga miradi ya umwagiliaji kama Wizara, watu wa kwanza ambao tunawapa kipaumbele ni watu ambao wanamiliki maeneo ambayo mradi unapita. Kwa hiyo, awaondoe shaka wananchi wa Bukoba, katika maeneo ambayo nimeyaainisha hapa wao ndio watakaokuwa kipaumbele namba moja mradi huu utakapokuwa umekamilika. (Makofi)

Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu kulipa kipaumbele zao la kahawa, sehemu ya mradi inatekeleza hiyo, lakini vilevile nimthibitishie tu kwamba sisi Wizara ya Kilimo mpaka sasa hivi tumenunua magari 18 kwa ajili ya kuchimba visima ambavyo vitakwenda kwenye hayo mashamba ya wakulima, hususan wakulima wa kahawa na mazao mengine kwa ajili ya kuongeza tija. Kwa hiyo, lipo katika mipango yetu na utekelezaji unaendelea. (Makofi)