Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 29 | Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives | Wizara ya Kilimo | 370 | 2025-05-21 |
Name
Charles John Mwijage
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Muleba Kaskazini
Primary Question
MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO K.n.y. MHE. CHARLES J. P. MWIJAGE aliuliza: -
Je, nini mawanda ya Mradi wa Bonde la Mto Ngono lililofanyiwa upembuzi yakinifu ili liweze kuendelezwa na lini ujenzi wa Mradi huo utaanza?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Bonde la Mto Ngono ni miongoni mwa mabonde 22 ya kimkakati ambayo yamefanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya kuendeleza kilimo cha umwagiliaji. Bonde hili linajumuisha maeneo ya umwagiliaji ya Wilaya za Bukoba, Misenyi na Muleba, zikiwemo Skimu za Kyabaramba, Katoro, Ngarama, Kyakakera, Kabaijuga, Kaibanja, Kishege, Minazi, Buterankuzi (Bukoba), Nkenge, kafunjo, Butulage, Buchurago, Bulembo Kusini (Misenyi), Ikondo, Buyaga, Buhangaza, Muhutwe, Katoke, Kagoma na Kikuku (Muleba). Aidha, eneo linalofaa kwa kilimo cha umwagiliaji katika bonde hili ni zaidi ya hekta 16,000.
Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Kilimo kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji imekamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na mchakato wa manunuzi kwa ajili ya kupata wakandarasi wa ujenzi wa skimu katika bonde hili unaendelea. Ujenzi wa skimu za Mto Ngono unatarajiwa kuanza mwaka huu wa fedha baada ya hatua za manunuzi kukamilika.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved