Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Ally Anyigulile Jumbe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyela

Primary Question

MHE. ALLY A. J. M. JUMBE aliuliza: - Je, lini Miradi ya Maji katika Wilaya ya Kyela itakamilika?

Supplementary Question 1

MHE. ALLY A. J. M. JUMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa majibu ya Serikali na niipongeze Serikali kwa kuendelea kutekeleza miradi mingi sana pale Wilayani Kyela. Pamoja na miradi hiyo na juhudi za Serikali, nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwenye Mradi wa Sinyanga Group. Mradi huu mpaka sasa hivi una miaka miwili na umefikia 15% tu, bado Serikali haijapeleka vifaa. Je, ni mbinu na muujiza gani utatumika kuhakikisha mradi huu unakamilika Disemba, mwaka 2025?

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili. Mradi wa Ngana Group ambao utanufaisha wananchi wengi sana, zaidi ya 66,000 kwenye kata saba na wananchi hao wanategemea kupata maji, upo 50% tu. Ni nini Kauli ya Serikali kwenye mradi huo?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana na pia, namshukuru sana Mheshimiwa Mbunge wa Kyela, kaka yangu, Mheshimiwa Ally Jumbe Mlaghila. Ni kweli kabisa miradi hii amekuwa akiisemea sana na bahati nzuri ameshafika ofisini kuifuatilia, kuangalia utekelezaji unaendaje.

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kabisa kwamba, Mradi wa Sinyanga upo 15% na Mradi wa Ngana upo 50%, kama alivyosema Mheshimiwa Mbunge. Tunatambua kabisa kwamba, wakati wa utekelezaji wake pale mwanzoni tulikuwa na changamoto, lakini pia, kulikuwa na mambo ya miundombinu, iliyokuwa inajengwa ilikuwa inapitia wakati mgumu kutokana na ushirikishwaji wa wananchi. Baada ya kugundua haya, tukaanza kufanya ushirikishwaji wa wananchi na baada ya hapo mradi ndiyo umeanza kukimbia sana.

Mheshimiwa Naibu Spika, nimtoe hofu. Disemba, 2025 mradi huu kwa sababu, fedha zipo na wataalamu wetu wameshapewa maelekezo na Serikali kuhakikisha kwamba unakamilika, ndiyo maana majibu yangu ya msingi ni kwamba, mradi utakamilika Disemba, 2025. Ahsante.

Name

Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Ilemela

Primary Question

MHE. ALLY A. J. M. JUMBE aliuliza: - Je, lini Miradi ya Maji katika Wilaya ya Kyela itakamilika?

Supplementary Question 2

MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Ningependa kumwuliza Mheshimiwa Waziri, Mradi wa Kuunganisha Majitaka katika maeneo ya milima, eneo la Manispaa ya Ilemela, waliunganisha kaya 390 Eneo la Kilimahewa A na B na wakasema kutakuwa na Mradi wa Awamu ya Pili, ambayo itakwenda kuunganisha Nyamanoro, Kirumba na kumalizia Kilimahewa yote. Je, lini mradi huu utaanza ili kuunganisha miundombinu ya majitaka maeneo ya milima? (Makofi)

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, ninapenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Angeline Mabula, Mbunge wa Ilemela, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kabisa awamu ya kwanza ilienda Kilimahewa lakini ni kaya 390 ziliunganishwa, lakini pia kulikuwa na Ibungilo. Sambamba na hivyo, tuna awamu ya pili ambayo tayari tumeshatangaza tender, mkandarasi ameshapatikana na mwezi wa Saba tunaenda kusaini mkataba kwa ajili kuanza awamu ya pili ambayo itaenda Kirumba, Nyamanoro pamoja na Kilimahewa ambapo zaidi ya kaya 1,600 zitaunganishwa na mfumo huo wa majitaka ili kuyaondoa katika makazi ya watu. Ahsante sana.