Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 29 Water and Irrigation Wizara ya Maji 369 2025-05-21

Name

Ally Anyigulile Jumbe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kyela

Primary Question

MHE. ALLY A. J. M. JUMBE aliuliza: -

Je, lini Miradi ya Maji katika Wilaya ya Kyela itakamilika?

Name

Kundo Andrea Mathew

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bariadi Mjini

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2024/25, Serikali imekamilisha utekelezaji wa Mradi wa Maji Lema, ambapo unanufaisha wananchi 3,357 waishio kwenye Kijiji cha Lema, kilichopo Wilayani Kyela, Mkoa wa Mbeya. Vilevile, Serikali inaendelea na utekelezaji wa Miradi Minne ya Ngana, Sinyanga, Kyela - Kasumulu na Ipinda, wilayani humo, ambayo ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Miradi hiyo inatarajiwa kukamilika mwezi Disemba, 2025 na kunufaisha zaidi ya wananchi 110,000 waishio kwenye maeneo ya vijiji na Mitaa ya Wilayani Kyela.