Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Mohamed Lujuo Monni

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Chemba

Primary Question

MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka walimu wa kike katika shule ambazo hazina walimu wa kike Wilayani Chemba?

Supplementary Question 1

MHE. MOHAMED L. MONNI: Mheshimiwa Naibu Spika, miaka minne hii mmeongeza idadi kubwa sana ya shule za msingi na sekondari, lakini pia, tumejenga madarasa mengi sana. Hii inatafsiri kwamba, idadi ya walimu imekuwa ndogo sana. Nataka kujua mkakati wa haraka wa kuendana na kasi hii ya ujenzi wa shule za msingi na sekondari ambazo zimejengwa? Ahsante.

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kabisa kutokana na utaratibu wa Elimu Bila Malipo, wazazi wengi wamehamasika kuwapeleka watoto wao shule, na kwa hakika udahili umeongezeka mara dufu. Ndiyo maana utaona kwamba, uhitaji wa madarasa umeongezeka na ndiyo maana Serikali imetumia, katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita, shilingi trilioni 5.1 kufanya uwekezaji katika sekta hii muhimu kabisa ya elimu msingi, kujenga madarasa na imefanya maendeleo mbalimbali katika miundombinu, kwa ajili ya kuwezesha kupokea wanafunzi hao wengi.
Mheshimiwa Naibu Spika, kama alivyosema Mheshimiwa Mohamed Monni, ongezeko la udahili huu pia limesababisha uhitaji wa walimu zaidi na utaona mikakati hii ya Serikali. Mkakati wa kwanza wa kuongeza walimu ni kuajiri. Serikali imekuwa ikiajiri waalimu kila mwaka wa fedha. Utaona kwamba, katika mwaka wa fedha tulionao, 2025/2026, walimu 15,925 wameajiriwa na tumepata taarifa kwamba, Serikali imetoa kibali cha kuongeza walimu wengine zaidi ya 10,000. Utaona kwamba, katika kipindi cha miaka minne walimu ambao wameajiriwa ni 45,742. Huu ni mkakati wa kwanza ambao ni kuajiri walimu.

Mheshimiwa Naibu Spika, mkakati wa pili ni matumizi ya TEHAMA, ambapo sasa Serikali inatumia madarasa janja kufanya ufundishaji mubashara. Yaani mwalimu anakuwa yupo eneo moja anatumia TEHAMA kufundisha wanafunzi katika maeneo tofauti tofauti kwa utaratibu unaoitwa ufundishaji mubashara.

Mheshimiwa Naibu Spika, lakini mkakati mwingine ni kutumia walimu kwa utaratibu wa mkataba.

NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri, kwa ufupi.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, utaratibu mwingine ni kutumia walimu wa kujitolea na pia, wale walimu ambao wapo katika mafunzo kwa vitendo. Kwa hiyo, Serikali itaendelea na mikakati hii, kuendelea kuongeza walimu ili wanafunzi wetu hawa waweze kupata walimu wa kutosha, waweze kuwapa elimu iliyo bora. Hiyo kazi inafanyika na Serikali ya Awamu ya Sita.

Name

Hawa Mchafu Chakoma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza: - Je, lini Serikali itapeleka walimu wa kike katika shule ambazo hazina walimu wa kike Wilayani Chemba?

Supplementary Question 2

MHE. HAWA M. CHAKOMA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi, ili niweze kuuliza swali. Ukosefu wa walimu wa kike katika Shule za Wilaya ya Chemba unafanana kabisa na Shule za Chalinze, Wilayani Bagamoyo. Je, ni lini Serikali itatupelekea walimu wa kike?

Name

Zainab Athuman Katimba

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimpongeze Mheshimiwa Hawa Mchafu, kwa kweli, amekuwa akifanya ufuatiliaji wa mara kwa mara na kuzungumzia sekta hii muhimu kabisa ya elimu msingi. Kuhusiana na swali lake, kuhusu walimu hawa wanawake, naomba nimhakikishie kwamba, Serikali inaendelea na utaratibu wa kuajiri walimu na tunazingatia pia, upatikanaji wa walimu wanawake, ambao tutawapanga katika vituo mbalimbali, ikiwemo katika mkoa ambao anatoka Mheshimiwa Hawa Mchafu.