Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 29 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 367 | 2025-05-21 |
Name
Mohamed Lujuo Monni
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Chemba
Primary Question
MHE. MOHAMED L. MONNI aliuliza: -
Je, lini Serikali itapeleka walimu wa kike katika shule ambazo hazina walimu wa kike Wilayani Chemba?
Name
Zainab Athuman Katimba
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. ZAINAB A. KATIMBA) alijibu: -
Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Chemba ina shule za msingi 113 na shule za sekondari 29. Aidha, shule zisizo na walimu wanawake ni shule za msingi 11 na shule za sekondari zote zina walimu wanawake.
Mheshimiwa Naibu Spika, mnamo Februari na Machi, 2025, Serikali imeajiri walimu 15,925 ambapo Halmashauri ya Chemba imepokea walimu 93 wa (awali na msingi 40 na sekondari 53) wakiwemo walimu 32 wanawake na walimu 61 wanaume. Shule tatu za msingi ambazo ni miongoni mwa shule ambazo hazikuwa na walimu wanawake zimepangiwa walimu hao.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kuajiri walimu, wakiwemo walimu wanawake, kadiri ya upatikanaji wa fedha.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved