Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Stella Simon Fiyao

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha maboma yaliyojengwa na Wananchi katika Mkoa wa Songwe?

Supplementary Question 1

MHE. STELLA S. FIYAO: Mheshimiwa Naibu Spika, ninashukuru sana kwa kunipa nafasi niulize maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri, lakini nataka kujua, wananchi wa Mkoa wa Songwe wamekuwa na mwamko mkubwa sana kuhakikisha wanajenga maboma yaliyo katika elimu na afya. Mwamko huo umepelekea Serikali kutoyakamilisha kwa wakati na kutokana na changamoto ya mvua ambazo zinaendelea kunyesha ndani ya mkoa wetu wa Songwe, maboma mengine mpaka yanaanguka na mvua. Sasa nataka kujua, mkakati wa Serikali ni upi kuhakikisha mnaongeza kasi ili kutowakatisha tamaa wananchi ambao wamejitoa kwa moyo kabisa? (Makofi)
Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu namba mbili. Nilitaka kujua mkakati wa Serikali ni upi kuhakikisha mnakarabati Shule ya Msingi Ileya iliyoko ndani ya Wilaya ya Ileje Kata ya Ndola? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Ni kweli kwamba Jimbo la Lulindi ni moja ya majimbo ambayo yana shule chakavu. Mheshimiwa Mbunge wa NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Katika kipindi cha miaka hii minne ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, Waheshimiwa Wabunge na wananchi wote wa Tanzania ni mashahidi, kazi kubwa sana imefanyika ya kujenga na kukamilisha maboma yaliyoanzishwa kwa nguvu za wananchi.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mfano, kwa Sekta ya Afya, maboma zaidi ya 1,000 ya zahanati yamekamilishwa na zahanati zimeanza kutoa huduma. Pia katika Sekta ya Elimu maboma mengi yamekamilishwa ya maabara na madarasa na yanaendelea kutoa huduma. Tumeendelea pia kujenga vituo katika maeneo mbalimbali.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, kwanza nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali ilisharatibu utaratibu wa kuainisha maboma yote kote nchini yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi na tuna idadi na tumendelea kuyatengea fedha kila bajeti kwa ajili ya kuhakikisha kwamba yanajengwa.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la msingi, ili maboma yasikae muda mrefu na kuharibika, tulishatoa maelekezo kwa Makatibu Tawala wa Mikoa na Wakurugenzi kote nchini kuratibu ujenzi wa maboma kwa awamu badala ya kujenga maboma yote kwa wakati mmoja na mengine yakakaa muda mrefu kabla hayajakamilika. Basi tunaendelea kuyaratibu yanajengwa kwa awamu ili Serikali iendelee kutenga fedha na kukamilisha maboma hayo.

Mheshimiwa Naibu Spika, jambo la pili kuhusiana na hiyo shule chakavu, Serikali kupitia Ofisi ya Rais, TAMISEMI imeendelea kukarabati shule kongwe na shule chakavu. Nikuhakikishie tu kupitia mradi wa boost na miradi mingine tutaendelea kuhakikisha kwamba tunatenga fedha kwa ajili ya kukarabati shule hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, nitumie nafasi hii nimwelekeze Mkurugenzi wa Halmashauri ya Ileje aweze kuwasilisha taarifa ya shule hiyo tuweze kuona mahitaji na Serikali iweze kutenga fedha kwa awamu kwa ajili ya ukarabati.

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha maboma yaliyojengwa na Wananchi katika Mkoa wa Songwe?

Supplementary Question 2

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Katika Jimbo la Bunda kuna Shule ya Masaba, Shule ya Chamtikiti, Shule ya Salagwa, na Nyasirori. Niliahidiwa kwamba hizi shule zitajengwa kwa kutumia mradi wa boost. Je, ni lini pesa za boost zitaenda kwenye shule hizo kuzikamilisha?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Utekelezaji wa mradi wa ukarabati wa shule na ujenzi wa shule kupitia programu mbalimbali ikiwemo boost na fedha nyingine za Serikali ni zoezi endelevu. Serikali inatambua kwamba katika Jimbo la Bunda Vijijini kwa Mheshimiwa Getere kuna uhitaji wa shule na yeye kama Mbunge alikwishawasilisha na Serikali inaendelea kufanya taratibu za kupata fedha kwa ajili ya kwenda kujenga na kukarabati shule hizo.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Getere kwamba Serikali inaendelea kuyafanyia kazi maombi ya Halmashauri hiyo ya Bunda Vijijini.

Name

Issa Ally Mchungahela

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Lulindi

Primary Question

MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha maboma yaliyojengwa na Wananchi katika Mkoa wa Songwe?

Supplementary Question 3

MHE. ISSA A. MCHUNGAHELA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Mwaka 2024 wakati tuna-wind-up, Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI aliniahidi shule tatu chakavu ambazo mpaka sasa hivi watoto wanasomea nje na Mheshimiwa Waziri alikuwepo akapewa maagizo hayo. Mpaka sasa hivi shule hizi chakavu sijazipata hata mojawapo. Wanasema nini kuhusiana na jambo hili? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Ni kweli kwamba Jimbo la Lulindi ni moja ya majimbo ambayo yana shule chakavu. Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo hilo, Mheshimiwa Mchungahela alishawasilisha, na Waziri wa Nchi alishatoa maelekezo kupitia kwa Katibu Mkuu na tumeshaainisha shule hizo. Kilichobaki sasa tunatafuta fedha kwa ajili ya kwenda kukarabati.

Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mchungahela kwamba zoezi hilo linaendelea, Serikali haijakaa kimya. Wakati wowote tukipata fedha hizo tutakuja kukarabati na kujenga shule hizo ili wananchi wa Lulindi wapate huduma za karibu katika Sekta ya Elimu.

Name

Suma Ikenda Fyandomo

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza: - Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha maboma yaliyojengwa na Wananchi katika Mkoa wa Songwe?

Supplementary Question 4

MHE. SUMA I. FYANDOMO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa swali dogo la nyongeza. Je, ni lini Serikali itapeleka fedha za umaliziaji maboma mawili kwenye shule ya Sekondari ya Isongole iliyopo Wilayani Rungwe? (Makofi)

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Serikali imekuwa ikiainisha maboma ambayo yanahitaji kukamilishwa katika shule mbalimbali za msingi na sekondari ikiwemo Shule ya Sekondari ya Isongole ambako Mheshimiwa Mbunge Fyandomo amesema.

Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge na nitumie nafasi hii nimwelekeze Mkurugenzi wa Halmashauri aweze kuainisha uwezo wa halmashauri yenyewe kukarabati na kukamilisha madarasa hayo kwa wakati, na ikiwa fedha za mapato ya ndani ya halmashauri hazitatosha, atupe taarifa ya gap la fedha ambayo inahitajika ili Ofisi ya Rais, TAMISEMI ione uwezekano wa kupeleka fedha. Lengo ni kuhakikisha kwamba madarasa hayo yamekamilika na yanatoa huduma zinazostahili.