Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 29 | Regional Administration and Local Government Authorities | Ofisi ya Rais TAMISEMI. | 365 | 2025-05-21 |
Name
Stella Simon Fiyao
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. STELLA S. FIYAO aliuliza: -
Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha maboma yaliyojengwa na Wananchi katika Mkoa wa Songwe?
Name
Dr. Festo John Dugange
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Wanging'ombe
Answer
NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:-
Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2020/2021 hadi 2023/2024, Serikali imepeleka jumla ya shilingi bilioni 156.5 kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma ya elimu na zahanati kote nchini ambapo kwa kipindi hicho, jumla ya shilingi bilioni 4.68 zimetumika kukamilisha maboma 51 ya zahanati na maboma 211 ya elimu katika Mkoa wa Songwe.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2024/2025, Serikali imetenga shilingi bilioni 9.54 kwa ajili ya kukamilisha maboma ya madarasa 734 ya shule za sekondari na msingi, matundu 114 ya vyoo, nyumba za walimu sita na bweni moja. Aidha, Serikali imetenga shilingi bilioni 30.38 kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma ya zahanati 346 kote nchini, ambapo Mkoa wa Songwe umetengewa shilingi milioni 752.
Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2025/2026, Serikali imetenga shilingi bilioni 2.9 kwa ajili ya kukamilisha maboma ya madarasa 209 ya shule za sekondari na msingi, matundu 66 ya vyoo, mabweni mawili na maabara 12 za shule za sekondari katika Mkoa wa Songwe.
Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali itaendelea kutenga fedha kwa awamu kwa ajili ya ukamilishaji wa maboma yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi kote nchini.
Copyright © Bunge Polis 2026. All Rights Reserved