Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Cecilia Daniel Paresso

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. CECILIA D. PARESSO K.n.y. MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA aliuliza: - Je, lini Serikali itamwomba Mwekezaji wa Chai Rungwe kuachia ardhi ambayo haitumii kwa wananchi?

Supplementary Question 1

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru. Ninaomba kuuliza swali moja la nyongeza. Pamoja na majibu haya ya Serikali, Mheshimiwa Mbunge pia alipenda kufahamu kwamba, ingawa eneo linatumika, bado kuna uhitaji wa wananchi wengine kupata eneo hilo. Hata hivyo, kuna sheria inayoruhusu, je, Serikali haioni sasa ni wakati mwafaka wa kufikiria kuligawanya kwa wananchi?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer


NAIBU WAZIRI WA AFYA, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, shamba hili linamilikiwa kihalali kabisa na Mohamed Enterprises na hakuna taarifa rasmi kuwepo kwa maeneo ambayo yanaweza yakapunguzwa kutoka kwa mmliki. Labda tulichukuwe kwa ajili ya kwenda kulifanyia kazi na kuona maeneo hayo ambayo wananchi wanaweza wakapewa. Lakini vinginevyo lipo kwenye miliki halali kabisa ya Mohamed Enterprises.

Name

Deo Kasenyenda Sanga

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Makambako

Primary Question

MHE. CECILIA D. PARESSO K.n.y. MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA aliuliza: - Je, lini Serikali itamwomba Mwekezaji wa Chai Rungwe kuachia ardhi ambayo haitumii kwa wananchi?

Supplementary Question 2

MHE. DEO K. SANGA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Kwa kuwa Mkoa wa Njombe na Mkoa wa Iringa, Kijiji cha Nyigu ambacho kipo Wilaya ya Mufindi, GN ya Kijiji cha Nyigu inaonesha iko katika Mkoa wa Njombe. Je, Mheshimiwa Waziri yupo tayari kuja ili kuwaunganisha viongozi wa mikoa wote wawili ili aoneshe GN ya kijiji hicho kimilikiwe na Njombe kama ilivyo kwenye GN?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Tumelichukua jambo la Mheshimiwa Mbunge, na tuwaelekeze Kamishna wa Ardhi wa Taifa apange timu ya kwenda pale kwenye mipaka ya Iringa na Njombe ili kwenda kuiweka sawa hali hiyo ili kumaliza utata uliopo katika ya mikoa hii miwili.

Name

Joseph George Kakunda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Sikonge

Primary Question

MHE. CECILIA D. PARESSO K.n.y. MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA aliuliza: - Je, lini Serikali itamwomba Mwekezaji wa Chai Rungwe kuachia ardhi ambayo haitumii kwa wananchi?

Supplementary Question 3

MHE. JOSEPH G. KAKUNDA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Katika Wilaya ya Sikonge, kwa mujibu wa bajeti ambayo tunayo sasa hivi tunaendelea nayo, Serikali ilikuwa imeleta hapa Bungeni maombi tupitishe bajeti ya kupima vijiji vyote 65 vilivyokuwa vimebaki, lakini mpaka sasa hivi fedha iliyotolewa ni ya kupima vijiji 16 tu na bado wiki mbili ili Bunge livunjwe. Je, tuna uhakika wa kupata hiyo fedha kweli ya kupima vijiji vyote 65 mwaka huu? (Makofi)

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, kwa mwaka huu wa fedha ambao unaisha wiki moja inayokuja, siyo rahisi kusema tutaleta fedha hizi katika kipindi hiki, lakini tushukuru kwamba katikati hapo tulipata karibu shilingi bilioni tano ambayo tumeitawanya nchi nzima angalau kugusa kidogo kidogo.

Mheshimiwa Spika, ninamwomba Mheshimiwa Mbunge kwamba kwenye bajeti ijayo tumetenga; vilevile kupitia tume tutaendelea na mpango wetu wa kukamilisha vijiji vyote katika jimbo la Mheshimiwa Mbunge. (Makofi)

Name

Dr. Christina Christopher Mnzava

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. CECILIA D. PARESSO K.n.y. MHE. SOPHIA H. MWAKAGENDA aliuliza: - Je, lini Serikali itamwomba Mwekezaji wa Chai Rungwe kuachia ardhi ambayo haitumii kwa wananchi?

Supplementary Question 4

MHE. DKT. CHRISTINA C. MNZAVA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa kumekuwa na migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji, na kuna wawekezaji wengi wakubwa wamewekeza na hawaendelezi yale maeneo, je, Serikali haioni kuna umuhimu wa kuwagawia wahitaji yale maeneo ambayo hayajaendelezwa? (Makofi)

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, nadhani ni kama wiki sasa tumejibu mwelekeo, nini tunafanya katika Wizara ya Ardhi. Tumeunda timu ya ufuatiliaji wa uendelezaji wa haya mashamba na yale yatakayobainika kwamba yametelekezwa na hayana uendelezaji wowote, Serikali inapanga kuyarejesha mikononi mwake, na wazo sasa kwenda kwa wananchi litafuata baada ya kuwa tumekamilisha hii hatua ambayo tunaendelea nayo. (Makofi)