Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Cecilia Daniel Paresso
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza: - Je, Serikali imejipangaje kutatua changamoto zilizojitokeza wakati wa ununuzi wa mbegu za ruzuku kwa wakulima nchini?
Supplementary Question 1
MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Kwanza, niipongeze Serikali kwa utaratibu huu mpya wa kutoa ruzuku kwa mbegu za mahindi.
Mheshimiwa Spika, swali la kwanza. Changamoto nyingine ambayo wanakutana nayo wananchi ni pale wanapoenda kwa mawakala kunapewa mbegu iliyopo na siyo mbegu wanayoihitaji. Nini mkakati wa Serikali kuhakikisha kwamba aina zote za mbegu kulingana na uhitaji inapatikana pindi ambapo mkulima anaenda?
Mheshimiwa Spika, swali la pili. Kampuni za mbegu zimekuwa na masharti magumu hivyo kuwafanya mawakala kushindwa kukidhi yale masharti kiasi kwamba inasababisha idadi ya mawakala kwenye wilaya zetu kuwa wachache kulingana na hayo masharti. Je, Serikali haioni ipo haja sasa kuangalia haya masharti yanayowekwa na makampuni makubwa ili kuyapunguza na kuwawezesha mawakala wengi waingie kusambaza mbegu hizi ili kuhakikisha upatikanaji wa mbegu mpaka maeneo ya vijijini?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, nami nimpongeze Mheshimiwa Cecilia Daniel Paresso kwa kufuatilia jambo hili kuhusiana na masuala ya mbegu. Pia nimthibitishie tu kwamba moja ya maelekezo ambayo Wizara tumeyatoa kwa mawakala ni kuhakikisha katika vituo vyao kunakuwa na mbegu za aina zote ili mkulima anapohitaji mbegu hiyo aweze kupatiwa ile ambayo inatokana na aina za mbegu ambazo zinapatikana katika eneo lake. Kwa hiyo, hilo ni eneo ambalo maelekezo tuliyatoa na tumeshawaelekeza TOSCI kufuatilia.
Mheshimiwa Spika, kuhusu masharti, ndiyo maana katika jibu la msingi utaona nimejibu hapo kwamba moja ya maelekezo ambayo tumeyapa makampuni ni kuhakikisha yanaongeza idadi ya mawakala. Kwa hiyo, makampuni yenyewe, cha kwanza wanapaswa kuwa na mawakala wao katika maeneo mbalimbali ili lile suala la kwamba sijui hujatimiza vigezo na nini, tuweze kuliondoa. Kwa hiyo, jambo hilo tumeshawaelekeza, lakini vilevile waweze kuwachunguza wale mawakala wapya ambao wanatosha na wana vigezo kwa ajili ya kusambaza mbegu hii. Kwa hiyo, hayo ni sehemu ya maelekezo na tumeshayatoa, ahsante.
Name
Festo Richard Sanga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Makete
Primary Question
MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza: - Je, Serikali imejipangaje kutatua changamoto zilizojitokeza wakati wa ununuzi wa mbegu za ruzuku kwa wakulima nchini?
Supplementary Question 2
MHE. FESTO R. SANGA: Mheshimiwa Spika, ninaipongeza Serikali kwa kutupatia ruzuku ya mbegu ya ngano kwa wananchi kwa Jimbo la Makete. Swali langu, wananchi hawa wamekuwa wakilima na mliwahakikishia kwamba somo litakuwepo, lakini wanunuzi wamekuwa wakinunua ngano na hawalipi kwa wakati. Ni ipi kauli ya Serikali ili wananchi wetu waweze kulipwa hasa wa Kata ya Kigala, Lupila na Ikuwa?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ninampongeza sana Mheshimiwa Festo Sanga kwa kazi nzuri anayofanya katika Jimbo lake la Makete, na ninajua moja ya watu ambao wamefanya kazi kubwa katika mpango huu wa ruzuku ya ngano ni pamoja na Mheshimiwa Festo. Nimthibitishie tu kwamba maelekezo ambayo Mheshimiwa Waziri ameyatoa wiki iliyopita, ni makampuni yote ambayo yanahitaji kuagiza ngano kutoka nje ya nchi, moja ya sharti la kwanza ni kuhakikisha wananunua ngano ya ndani ya nchi na kulipa kwa wakati.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, sisi tutaenda kuongeza usimamizi na ufuatiliaji ili wananchi wake walipwe kwa wakati. Kwa hiyo, jambo hilo tunaomba tulipokee na tukalifanyie kazi.
Name
Prof. Patrick Alois Ndakidemi
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Moshi Vijijini
Primary Question
MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza: - Je, Serikali imejipangaje kutatua changamoto zilizojitokeza wakati wa ununuzi wa mbegu za ruzuku kwa wakulima nchini?
Supplementary Question 3
MHE. PROF. PATRICK A. NDAKIDEMI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Tunaishukuru sana Serikali kwa kuwapatia wakulima wa Jimbo la Moshi Vijijini miche bora ya kahawa kwa kuwapa bure. Je, Serikali ina mkakati gani wa kuwasaidia wakulima hawa wapate viuatilifu bure au kwa bei ya ruzuku kwa sababu kuna uharibifu mkubwa sana unaotokana na wadudu?
Name
David Ernest Silinde
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Tunduma
Answer
NAIBU WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ninampongeza vilevile Prof. Ndakidemi ambaye amefanya kazi nzuri sana pale Moshi Vijijini na kufuatilia zao la kahawa. Nami ni moja ya watu ambao nilishiriki pamoja naye kugawa bure miche ya kahawa kwa mfumo wa ruzuku.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimthibitishie tu kwamba kwenye upande wa viuatilifu kama ambavyo tunafanya katika korosho, vilevile tutafanya katika kahawa kwa sababu mpango wa sasa ni kuhakikisha tunawawezesha wakulima kupunguza gharama za uzalishaji katika mazao yote ya kimsimu.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tumekuwa tukienda kwa awamu, tunatoka kwenye korosho tunakwenda kwenye kahawa na tutakwenda katika mazao mengine. Kwa hiyo, lipo katika sehemu ya mipango ya Serikali, ahsante.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved