Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 46 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 596 2025-06-16

Name

Cecilia Daniel Paresso

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. CECILIA D. PARESSO aliuliza: -

Je, Serikali imejipangaje kutatua changamoto zilizojitokeza wakati wa ununuzi wa mbegu za ruzuku kwa wakulima nchini?

Name

David Ernest Silinde

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tunduma

Answer

NAIBU WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Spika, usambazaji wa mbegu za mahindi kwa mpango wa ruzuku ulianza msimu wa 2024/2025. Katika utekelezaji wa mpango huo, Serikali imebaini changamoto mbalimbali ikiwemo wakulima kukosa namba ya usajili ya ruzuku; bei elekezi ya ruzuku kushindwa kutekelezwa kwa wauzaji wadogo walioko katika ngazi za kata na vijiji; baadhi ya mawakala na makampuni ya mbegu wasio waaminifu kuuza mbegu nje ya mfumo wa ruzuku; na idadi ndogo ya wauzaji wa mbegu hususan katika ngazi za kata na vijiji.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza kuchukua hatua mbalimbali ili kukabiliana na changamoto hizo kwa ajili ya msimu wa 2025/2026. Hatua hizo ni kuhakikisha wakulima wa zao la mahindi wanasajiliwa kwa wakati katika mfumo wa pembejeo za kilimo; kutoa elimu kwa umma kuhusu utekelezaji wa mpango wa ruzuku ya mbegu za mahindi; kufanya mapitio ya bei elekezi ya mbegu inayotumika ili kuwezesha mawakala wadogo kuingizwa kwenye mfumo wa ruzuku; kuchukua hatua kali kwa mawakala wa mbegu watakaouza mbegu za mahindi bila kufuata bei elekezi ya ruzuku; na kuzielekeza Kampuni za mbegu kuongeza idadi ya mawakala wa mbegu wanaosambaza mbegu za ruzuku hususan vijijini.