Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Aloyce John Kamamba

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kakonko

Primary Question

MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza: - Je, lini Wilaya ya Kakonko itakuwa na Wakala wa Mamlaka ya Maji Mjini katika Mji wa Kakonko?

Supplementary Question 1

MHE. ALOYCE J. KAMAMBA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi, aidha nashukuru sana kwa majibu mazuri ya Serikali. KAUWASA kwa maana ya Mamlaka ya Maji katika Mji wa Kakonko unahudumia Kata za Kanyonza, Kasuga, Kiziguzigu, Kasanda na Kakonko. Vyanzo vya maji ambavyo vinahudumia Mji wa Kakonko ni chanzo cha kutoka Kijiji cha Kasuga na chanzo cha Maji cha Kijiji cha Nyakayenzi.
Mheshimiwa Spika, katika vyanzo hivyo viwili, kinachofanya kazi ni chanzo cha maji cha Kasuga, lakini chanzo cha maji cha Nyakayenzi hakifanyi kazi pamoja na kwamba Serikali ilishapeleka fedha zaidi ya shilingi bilioni 2,800, kwa ambacho kinazungumzwa kwamba ni changamoto katika usanifu lakini na ujenzi. Nini kauli ya Serikali kuhakikisha kwamba mradi huo sasa unaokolewa ili uweze kufanya kazi uliyokusudiwa?

Mheshimiwa Spika, swali la pili, upo mradi wa maji wa Kijiji cha Kabale ambapo zaidi ya shilingi milioni 803 zimepelekwa pale, zilikusudiwa kupelekwa pale, lakini shilingi milioni 300 zimeshapelekwa, mradi haujakamilika tangu mwaka 2024 mwezi wa 12 ujenzi umesimama. Nini kauli ya Serikali kuonesha kwamba mradi sasa unaokolewa na unafanya kazi kama ambavyo ilikusudiwa tangu mwanzo? Ahsante.

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ninakiri tu kwamba Mheshimiwa Mbunge pamoja na kuuliza hili swali hapa lakini pia amefika ofisi za maji kufuatilia changamoto za mradi huu, nami kwenye swali lake la kwanza nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba baada ya kupokea hayo malalamiko, Wizara ya Maji imeshaandaa wataalam ambao watakwenda Wilaya ya Kakonko kwenda kuangalia changamoto na kufanya tathmini na waweze kushauri Serikali hatua za kufanya.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, kabla ya mwezi Julai wataalam hawa watakuwa wamefika katika Wilaya ya Kakonko ili kufanya hiyo tathmini na kushauri Serikali hatua za kufanya.

Mheshimiwa Spika, kuhusu hiki chanzo cha maji katika Kijiji cha Kabale ambacho bado hatujakamilisha kupeleka fedha, Serikali imepanga katika muhula wa kwanza wa mwaka wa bajeti, fedha zitapelekwa ili mradi huo uweze kukamilishwa ambao ulikuwa umesimama.