Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 46 Water and Irrigation Wizara ya Maji 595 2025-06-16

Name

Aloyce John Kamamba

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kakonko

Primary Question

MHE. ALOYCE J. KAMAMBA aliuliza: -

Je, lini Wilaya ya Kakonko itakuwa na Wakala wa Mamlaka ya Maji Mjini katika Mji wa Kakonko?

Name

Jumaa Hamidu Aweso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Pangani

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI K.n.y. WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, katika kuongeza ufanisi wa utoaji wa huduma ya majisafi na salama kwa wananchi, Serikali imeanzisha Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Kakonko (KAUWASA) ambayo inahudumia Kata tano za Kakonko, Kasuga, Kanyonza, Kiziguzigu na Kasanda. Usimamizi wa utoaji huduma chini ya Mamlaka hiyo ulianza rasmi mwezi Septemba, 2024.