Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Abdallah Dadi Chikota

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyamba

Primary Question

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA K.n.y. MHE. KATANI A. KATANI aliuliza:- Je, lini Serikali itawalipa Wakandarasi wa Miradi ya Maji fedha zao kutokana na miradi mingi kutokamilika kwa kukosa malipo kwa wakati?

Supplementary Question 1

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Pamoja na kwamba Serikali inatafuta fedha kumalizana na wakandarasi, lakini kuna wakandarasi wawili; mmoja anajenga mradi wa Makonde ambao unahudumia halmashauri nne; Newala Mjini, Newala Vijijini, Tandahimba na Nanyamba, yeye ana madai ya muda mrefu na bado hayajashughulikiwa na mkandarasi ambaye anaboresha mradi wa Mnyawi kwenda Nanyamba na yeye ana madai ya muda mrefu.

Je, Serikali haioni umuhimu sasa wa kuwalipa wakandarasi hawa ili waendelee na kazi yao ya kutekeleza miradi na hatimaye wananchi wapate maji ambayo ni shida yao ya siku nyingi?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, tunakiri kwamba wakandarasi hao wawili ni wakandarasi ambao wamefanya kazi nzuri sana. Nimwahidi Mheshimiwa Mbunge na hao wakandarasi pamoja na wananchi ambao watapata hiyo huduma kwamba Serikali imejipanga kuhakikisha kwamba tunapoanza tu muhula wa kwanza, kwa maana ya quarter ya kwanza ya mwaka wa bajeti, wakandarasi hao watalipwa fedha yao, ahsante.

Name

Kavejuru Eliadory Felix

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Buhigwe

Primary Question

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA K.n.y. MHE. KATANI A. KATANI aliuliza:- Je, lini Serikali itawalipa Wakandarasi wa Miradi ya Maji fedha zao kutokana na miradi mingi kutokamilika kwa kukosa malipo kwa wakati?

Supplementary Question 2

MHE. KAVEJURU E. FELIX: Mheshimiwa Spika, kule Buhigwe tuna mradi wa vijiji nane ambao unatekelezwa na mzabuni Rukolo, muda wa ukamilishaji wa mradi huo umeshapita na mkandarasi huyo bado anadai fedha nyingi zaidi ya shilingi bilioni mbili na mradi umesimama. Lini atalipwa fedha zake ili akamilishe huo mradi kwa sababu muda wa ukamilishaji wa mradi huu umeshapita?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba kama nilivyojibu katika jibu la msingi, tunatambua kazi nzuri ambayo amefanya huyo mkandarasi na Serikali ilishapokea hati yake ya madai kuhakikisha kwamba analipwa. Pia nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba Serikali inaandaa malipo ili aweze kumlipa mkandarasi na aweze kukamilisha hiyo kazi ambayo bado haijakamilika hadi mwisho.