Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 46 Water and Irrigation Wizara ya Maji 594 2025-06-16

Name

Katani Ahmadi Katani

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tandahimba

Primary Question

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA K.n.y. MHE. KATANI A. KATANI aliuliza:-

Je, lini Serikali itawalipa Wakandarasi wa Miradi ya Maji fedha zao kutokana na miradi mingi kutokamilika kwa kukosa malipo kwa wakati?

Name

Jumaa Hamidu Aweso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Pangani

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI K.n.y. WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea kulipa madeni ya wakandarasi, wataalam washauri na watoa huduma mbalimbali wanaotekeleza au kutoa huduma kwenye ujenzi wa miradi ya maji nchini ikiwemo Wilaya ya Tandahimba. Hadi kufikia mwezi Mei, 2025, jumla ya shilingi 2,548,920,536.19 kati ya shilingi 3,999,970,936.19 za madai ya wakandarasi na watoa huduma wanaotekeleza miradi mbalimbali ya maji Wilayani Tandahimba zimelipwa.

Mheshimiwa Spika, aidha, Serikali itaendelea kulipa madai yote ya wakandarasi, wataalam washauri na watoa huduma wa miradi ya maji nchini kadri fedha zinavyopatikana ili miradi hiyo iweze kukamilika kwa wakati na kuanza kutoa huduma iliyokusudiwa kwa wananchi, ahsante.