Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Margaret Simwanza Sitta

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Urambo

Primary Question

MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza: - Je, lini Geti la kuingilia Watalii Hifadhi ya Mto Ugala Wilaya ya Urambo litawekwa?

Supplementary Question 1

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Serikali nilikuwa na swali moja la nyongeza kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa eneo kubwa la hifadhi ambalo linatumika na watalii lipo upande wa Usoke, je, ni lini Serikali itajenga barabara nzuri ili kuwezesha watalii waingie kwenye hifadhi kwa kupitia Usoke? (Makofi)

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Mheshimiwa Spika, kama nilivyojibu kwenye swali la msingi, tunaiendeleza mbuga hii kwa awamu, na awamu ya kwanza zimetolewa shilingi bilioni mbili ambazo kama nilivyojieleza zinaendelea kuchakata kwenye maeneo haya ya maboresho ya hifadhi yetu.

Mheshimiwa Spika, kutegemeana na fedha zitakavyoendelea kupatikana kwa awamu ya pili inayokuja, jambo la Mheshimiwa Mbunge litachukuliwa umuhimu wa kipekee kuona kwamba lango la Usoke linafunguliwa.