Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
| Term | Session | Sitting | Sector | Ministry | Qn No | Date |
|---|---|---|---|---|---|---|
| 2020-2025 | Session 19 | Sitting 46 | Natural Resources and Tourism | Wizara ya Maliasili na Utalii | 593 | 2025-06-16 |
Name
Margaret Simwanza Sitta
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Urambo
Primary Question
MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza: -
Je, lini Geti la kuingilia Watalii Hifadhi ya Mto Ugala Wilaya ya Urambo litawekwa?
Name
Dr. Pindi Hazara Chana
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Answer
NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII alijibu: -
Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kuwa Hifadhi ya Taifa ya Mto Ugala inakuwa miongoni mwa Hifadhi bora nchini, Serikali imepanga kuiendeleza Hifadhi hiyo kwa awamu ambapo katika awamu ya kwanza Serikali imetumia shilingi 2,000,000,000.00 kuboresha miundombinu muhimu ya Hifadhi ikiwemo ujenzi wa mtandao wa barabara hifadhini, ujenzi wa jengo la utawala, nyumba za watumishi, vituo vya askari, visima vya maji na maeneo ya kupumzika wageni.
Mheshimiwa Spika, mara baada ya kukamilika kwa awamu hii, Serikali itajielekeza kwenye kujenga malango manne ambayo ni Lunyeta, Lumbe, Iluma na Izengabatogilwe kwa kadiri ya upatikanaji wa fedha.
Copyright © Bunge Polis 2025. All Rights Reserved