Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Janejelly Ntate James

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JANEJELLY J. NTATE K.n.y. MHE. MICHAEL M. KEMBAKI aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kutatua masharti kandamizi kwa wawekezaji wa ndani kama kukadiria na kulipa kodi kabla ya kuanza biashara?

Supplementary Question 1

MHE. JANEJELLY J. NTATE: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu ya Serikali na kuweka hiyo sheria, lakini swali la kwanza, hiyo sheria bado haijaanza kutekelezwa kwa wafanyabiashara, na bado haiendi kama inavyosema, miezi sita wanalipishwa kabla ya miezi sita.

Mheshimiwa Spika, pili, mwekezaji wa nje anapewa miaka mitano, na Mtanzania anapewa miezi sita, kutakuwa na ushindani wa uwiano? (Makofi)

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, kwanza, swali lake la kwanza nitoe maelekezo kwa Kamishna wa Mamlaka ya Mapato Tanzania wahakikishie kwamba watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania wanafuata taratibu na sheria ambayo imewekwa. Mtu anatakiwa alipe baada ya miezi sita tangu amepewa TIN.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, tofauti hii ambayo amezungumza, naomba tuichukue twende tukaifanyie kazi. Ushauri wake tutaenda kuuweka vizuri. (Makofi)

Name

Ng'wasi Damas Kamani

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JANEJELLY J. NTATE K.n.y. MHE. MICHAEL M. KEMBAKI aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kutatua masharti kandamizi kwa wawekezaji wa ndani kama kukadiria na kulipa kodi kabla ya kuanza biashara?

Supplementary Question 2

MHE. NG'WASI D. KAMANI: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana kwa kunipa nafasi hii ya kuuliza swali la nyongeza. Tumekuwa na maswali mbalimbali kwa kuhusiana na kigezo hiki cha wananchi kuchajiwa kodi kabla ya kuanza biashara na maafisa wetu wa kodi kukiuka kigezo hiki cha sheria cha kukusanya kodi kabla ya miezi sita; na Mheshimiwa Waziri amekuwa akitoa majibu haya, na kutoa maelekezo haya kwa watu wa TRA ili kuhakikisha sheria hii inafuatwa na kutekelezwa kama ilivyo. Sasa maelekezo haya yamekuwa hayafanyiwi kazi. Nini kauli ya Serikali juu ya maafisa ambao wanaendelea kukiuka maelekezo ya Serikali katika kifungu hiki hata baada ya maelekezo kuwa yanatolewa? (Makofi)

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, kama nimejibu suala hili, lakini kwa nyongeza haigombi. Tunasema kwamba wale ambao hawatafuata sheria na taratibu, basi Sheria ya Kiutumishi itachukua mkondo wake. (Makofi)

Name

Neema Kichiki Lugangira

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. JANEJELLY J. NTATE K.n.y. MHE. MICHAEL M. KEMBAKI aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kutatua masharti kandamizi kwa wawekezaji wa ndani kama kukadiria na kulipa kodi kabla ya kuanza biashara?

Supplementary Question 3

MHE. NEEMA K. LUGANGIRA: Mheshimiwa Spika, katika muktadha huu huu wa kulinda na kuinua wawekezaji wa ndani, je, Serikali haioni iko haja ya kubadilisha sheria na kuona namna ambavyo itaweza kuwapatia wajasiriamali wadogo hususan vijana na wanawake ile likizo ya kutolipa kodi kama ambavyo wawekezaji wa nje wanapata ili waweze kurasimisha biashara zao?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, ushauri wake tumeupokea na tunaenda kuufanyia kazi. Tukiona ipo haja na tija ya kufanya hivyo, tutaleta Muswada huo katika Bunge lako Tukufu kwa ajili ya kupitisha sheria hiyo. (Makofi)

Name

Charles Muguta Kajege

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mwibara

Primary Question

MHE. JANEJELLY J. NTATE K.n.y. MHE. MICHAEL M. KEMBAKI aliuliza: - Je, Serikali ina mkakati gani wa kutatua masharti kandamizi kwa wawekezaji wa ndani kama kukadiria na kulipa kodi kabla ya kuanza biashara?

Supplementary Question 4

MHE. CHARLES M. KAJEGE: Mheshimiwa Spika, sharti hili ambalo linawabana wafanyabiashara kulipa kodi kabla hawajaanza kufanya biashara, kwa kweli ni mojawapo ya vigezo ambavyo vinafanya wafanyabiashara wengi washindwe kufanya biashara. Je, kwa nini Serikali isiondoe sharti hili?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA: Mheshimiwa Spika, Serikali imeweka sheria ambayo Bunge lako Tukufu limepitisha sheria hiyo. Kwa hiyo, cha msingi hapa ni kuhakikisha kwamba watumishi wetu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania na taasisi nyingine kufuata sheria na taratibu ambazo zimewekwa na Serikali.