Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 46 Finance Wizara ya Fedha 590 2025-06-16

Name

Michael Mwita Kembaki

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Tarime Mjini

Primary Question

MHE. JANEJELLY J. NTATE K.n.y. MHE. MICHAEL M. KEMBAKI aliuliza: -

Je, Serikali ina mkakati gani wa kutatua masharti kandamizi kwa wawekezaji wa ndani kama kukadiria na kulipa kodi kabla ya kuanza biashara?

Name

Hamad Hassan Chande

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kojani

Answer

NAIBU WAZIRI WA FEDHA alijibu: -
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Bunge lako Tukufu, ilifanya Marekebisho ya Sheria ya Usimamizi wa Kodi (Tax Administration Act, 2015) Kifungu cha 22, ili kuahirisha wajibu wa kulipa kodi ya awamu chini ya Sheria ya Kodi ya Mapato kwa kipindi cha miezi sita tangu tarehe ambayo Nambari ya Utambulisho ya Mlipaji (TIN) ilipotolewa kwa mtu yeyote anayesajiliwa na kupewa TIN kwa mara ya kwanza.

Mheshimiwa Spika, kwa mabadiliko haya, mfanyabiashara aliyesajiliwa kwa mara kwanza atalipa jumla ya kodi aliyoahirishiwa baada ya miezi sita kwa awamu tatu. Lengo la mabadiliko haya ya sheria ni kuweka mazingira wezeshi kwa wafanyabiashara na wawekezaji.