Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Boniphace Nyangindu Butondo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kishapu

Primary Question

MHE. BONIPHACE N. BUTONDO aliuliza: - Je, lini Serikali itatangaza tender ya ujenzi wa Km 20 kwa kiwango cha lami Barabara ya Kolandoto - Kishapu hadi Mwangongo?

Supplementary Question 1

MHE. BONIPHACE N. BUTONDO: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, kwanza, napongeza kwa majibu haya ya Serikali, lakini ninataka niseme yamekuwa ni majibu ya matumaini tu kila wakati. Ahadi ya mwaka huu wa fedha (mwaka 2025/2026) ilikuwa ni kutekeleza kilometa 20 za kiwango cha lami kati ya kilometa 52. Serikali ilifikia hatua ya kutangaza tender, lakini haijatangaza tatizo ni nini ama changamoto ni nini? (Makofi)

Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa mwaka mzima barabara hii tumekuwa tukitumia shilingi milioni 850 kwa ajili ya matengenezo ya kawaida, gharama ambayo ni kubwa sana. Sasa Serikali haioni kwamba ni wakati wa kutekeleza mradi huu katika kiwango cha lami ili kupunguza gharama kwa Serikali? (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ni kweli kama alivyosema tulikuwa tumepanga tuanze kuijenga hiyo barabara na taratibu zote zilikuwa zimekamilika na mpaka tunamaliza mwaka hatujaanza kuijenga, na ndiyo maana hata katika mwaka wa fedha unaokuja tumepanga barabara hii tuanze kuijenga kwa kiwango cha lami ambayo ninaamini tutaitangaza yote, japo tutaanza kujenga pia kulingana na upatikanaji wa fedha kama nilivyosema.

Mheshimiwa Spika, ninakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwamba nia ya Serikali ni kujenga barabara nyingi na hasa mojawapo hiyo ambayo ni barabara kuu kwa kiwango cha lami barabara zote zile kuu. Ndiyo maana mpaka sasa hivi tunaendelea, jitihada za Serikali ni kuzijenga barabara zote hizo lakini kabla hatujazijenga lazima tuendelee kuzikarabati hata kama ni kwa gharama ili ziweze kutoa huduma kwa wananchi.