Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 46 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 589 2025-06-16

Name

Boniphace Nyangindu Butondo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kishapu

Primary Question

MHE. BONIPHACE N. BUTONDO aliuliza: -

Je, lini Serikali itatangaza tender ya ujenzi wa Km 20 kwa kiwango cha lami Barabara ya Kolandoto - Kishapu hadi Mwangongo?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa barabara ya Kolandoto – Kishapu hadi Mwangongo yenye urefu wa kilometa 52.79 unatekelezwa kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Hadi sasa jumla ya kilometa 2.58 zimejengwa kwa kiwango cha lami katika Mji wa Mhunze (Kishapu). Aidha, Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuendelea na ujenzi wa sehemu iliyobaki, ahsante. (Makofi)