Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Robert Chacha Maboto

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda Mjini

Primary Question

MHE. ROBERT C. MABOTO aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Zimamoto katika Halmashauri ya Mji wa Bunda?

Supplementary Question 1

MHE. ROBERT C. MABOTO: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa nafasi. Nina swali moja la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Mji wa Bunda au Wilaya ya Bunda ina zaidi ya majimbo matatu ya uchaguzi na ina idadi kubwa sana ya watu. Je, Serikali katika mpango iliyonao katika orodha ya magari ambayo ilisema inayaleta kwa ajili ya zimamoto, Halmashauri ya Mji wa Bunda kwenye orodha hiyo imo?

Name

Geophrey Mizengo Pinda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kavuu

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Mheshimiwa Spika, kama ulivyotolewa mwongozo wa orodha ya magari yatakayosambazwa kwenye halmashauri, ninao uhakika Bunda ni moja kati ya Halmashauri zitakazopata magari.