Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 46 Home Affairs Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi 588 2025-06-16

Name

Robert Chacha Maboto

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda Mjini

Primary Question

MHE. ROBERT C. MABOTO aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga Kituo cha Zimamoto katika Halmashauri ya Mji wa Bunda?

Name

Innocent Lugha Bashungwa

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Karagwe

Answer

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI K.n.y. WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Robert Chacha Maboto, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na jitihada za kusogeza huduma za zimamoto na uokoaji karibu na wananchi kwa kujenga vituo vya zimamoto na uokoaji. Aidha, katika mwaka 2025/2026 Serikali kupitia Jeshi la Zimamoto na Uokoaji imetenga fedha kiasi cha shilingi milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa Kituo cha Zimamoto na Uokoaji katika Halmashauri ya Mji wa Bunda.