Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Rashid Abdallah Shangazi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlalo

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga upya barabara ya Mombo hadi Lushoto yenye kilometa 36 kwa kiwango cha lami ili kukidhi mahitaji ya sasa?

Supplementary Question 1

MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Spika, barabara hii imejengwa zaidi ya miaka 30 iliyopita na kwa kweli imejengwa katika vipimo vya kizamani ambavyo ni upana wa mita sita na hata jana barabara hii imepata changamoto maporomoko yameiziba kwa muda. Sasa kwa kuwa Serikali inakiri kwamba imeshafanya upembuzi wa kina na usanifu; je, ipo tayari kutafuta fedha kwa haraka ili kwenda kukarabati barabara hii?

Mheshimiwa Spika, swali la pili; kipande cha barabara kutoka Nyasa - Mlalo kwenda Majulai, mkandarasi alikuwepo site kwa muda lakini sasa ameondoka. Ningependa kujua hali ipoje sasa ni lini mkandarasi yule atarejea ili kwenda kuendelea na ujenzi katika kipande kile?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Ninaomba kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba barabara ya Mombo – Lushoto yenye urefu wa kilometa 36 ni ya zamani, ni nyembamba na ni barabara ambayo inapita kwenye miinuko mikali na mawe. Tunakiri kwamba imekuwa ni kawaida kila zinaponyesha mvua (eneo lina mvua nyingi sana) huwa kunakuwa na maporomoko ya mawe.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge tumeweka timu ya wataalamu ambao mpaka sasa hivi tunavyoongea wapo eneo hilo, kila mawe yanapoanguka kwa sababu ya ufinyu wa barabara huwa wanayaondoa.

Mheshimiwa Spika, Serikali tumeshafanya usanifu kwa ajili ya kuipanua hiyo barabara na tunatafuta chanzo cha uhakika kwa sababu hiyo barabara ndiyo barabara pekee ya muhimu inayoingia huko Lushoto ambako kuna uzalishaji mkubwa sana. Kwa hiyo Serikali tumeshafanya usanifu, tunatafuta chanzo cha uhakika ili kuweza kuipanua na kuiweka kwenye viwango vya sasa.

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala lake la pili, hii barabara ya kutoka Nyasa kwenda Majulai ni sehemu tu ya barabara ambayo inatoka Lukozi - Nyasa hadi Mng’alo, tunaijenga kwa awamu hatujasimama. Tayari tumejenga kilometa 2.8 na kilometa tatu ambazo tunaenda kuzijenga tayari tumeshapata mkandarasi na muda wowote tunasaini ili tukamilishe hizo kilometa tatu ambazo tutazifanya.

Name

Noah Lemburis Saputi Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Arumeru-Magharibi

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga upya barabara ya Mombo hadi Lushoto yenye kilometa 36 kwa kiwango cha lami ili kukidhi mahitaji ya sasa?

Supplementary Question 2

MHE. NOAH L. S. MOLLEL: Mheshimiwa Spika, barabara ya Mianzini – Sambasha – Ngaramtoni, mkandarasi amesimama kwa muda mrefu sasa hafanyi kazi yoyote. Je, ni lini Serikali itapeleka pesa kumpa mkandarasi huyo ili barabara hiyo iendelee kutengenezwa kwa sababu ni ya mjini?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Ukiachilia mbali hali ya mvua inayoendelea lakini ukweli ni kwamba mkandarasi huyo hajaondoka site ila amepunguza ile kasi ya kutengeneza hiyo barabara. Tayari tumeshapokea maombi yake na tunashughulikia hati za malipo ili aweze kuongeza kasi mara baada ya kumlipa fedha.

Name

Esther Lukago Midimu

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga upya barabara ya Mombo hadi Lushoto yenye kilometa 36 kwa kiwango cha lami ili kukidhi mahitaji ya sasa?

Supplementary Question 3

MHE. ESTHER L. MIDIMU: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali la nyongeza. Barabara ya kutoka Bariadi – Itilima – Kisesa – Meatu – Singida ipo kwenye Ilani. Je ni lini Serikali itajenga kwa kiwango cha lami? (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Barabara anayoisema ni ya mkoa na ninataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba ipo kwenye hatua za usanifu. Kwa hiyo ipo inasanifiwa ili iweze kuingia kwenye ujenzi kwa kiwango cha lami.

Name

Omari Mohamed Kigua

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kilindi

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI aliuliza: - Je, lini Serikali itajenga upya barabara ya Mombo hadi Lushoto yenye kilometa 36 kwa kiwango cha lami ili kukidhi mahitaji ya sasa?

Supplementary Question 4

MHE. OMARI M. KIGUA: Mheshimiwa Spika, barabara ya kutoka Handeni – Kibirashi – Songe sasa hivi magari yanatumia zaidi ya saa sita kwa sababu kwa mvua zinazonyesha maeneo mengi yana mashimo. Je, nini mpango wa Serikali wa kuhakikisha kwamba barabara hiyo inafanyiwa ukarabati ili iweze kupitika muda wote? (Makofi)

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Sambamba na swali la Mheshimiwa Kigua, maeneo mengi ya nchi ambapo mvua zinanyesha kwa kweli hasa hizi barabara za kiwango cha changarawe kulikuwa na changamoto kwa sababu ya mvua.

Mheshimiwa Spika, tumetenga fedha za matengenezo ikiwepo hiyo barabara ya Kibirashi kwenda Songe. Nimhimize tu Mheshimiwa, nimpe maelekezo Meneja wa Mkoa wa Tanga kuhakikisha kwamba anaweka timu katika eneo hilo ili kuweza kukwamua hayo magari tukisubiri mvua ikatike halafu tuweze kuikarabati kwa kiwango ambacho tunakihitaji.