Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 25 Works and Transport Wizara ya Ujenzi 329 2025-05-15

Name

Rashid Abdallah Shangazi

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mlalo

Primary Question

MHE. RASHID A. SHANGAZI aliuliza: -

Je, lini Serikali itajenga upya barabara ya Mombo hadi Lushoto yenye kilometa 36 kwa kiwango cha lami ili kukidhi mahitaji ya sasa?

Name

Eng. Godfrey Msongwe Kasekenya

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Ileje

Answer

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TANROADS, imekamilisha Upembuzi Yakinifu na Usanifu wa Kina wa barabara ya Mombo – Lushoto yenye urefu wa kilometa 36 kwa ajili ya kuifanyia ukarabati mkubwa kwa kiwango cha lami. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya kuanza ukarabati huu, ahsante.