Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Asha Abdullah Juma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA aliuliza: - Je, ni lini Serikali itaanzisha utaratibu wa kuwasajili waendesha bodaboda nchini?

Supplementary Question 1

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa majibu mazuri ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, tunatambua umuhimu wa sekta hii ya wanabodaboda inavyosaidia kuzalisha ajira kwa vijina. Ni jukumu la mamlaka kuhakikisha kwamba vijana hawa wanabaki salama lakini vijana wengi wanaendelea kupata ajali wengine wanapoteza maisha wanakuwa vilema.

Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha kwamba katika huo usajili vijana hawa wanapewa sharti la kwanza kwamba ni lazima watumie kofia ngumu wakati wanaposafirisha abiria?

Swali la pili, Je, Serikali ina mpango gani kuhakikisha kwamba ni lazima kila mwendesha (bodaboda) pikipiki awe amesajiliwa ili kuweza kuwaratibu vizuri na siyo jambo la hiari kama ulivyoeleza Mheshimiwa Waziri ili hawa watu wanaweza kuratibiwa vizuri? Ahsante. (Makofi)

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM: Mheshimiwa Spika, ninapenda kujibu swali la Mheshimiwa Asha, kwanza ninapenda atambue kuwa usajili wowote wa vyombo vya moto ambavyo vinaendeshwa barabara basi anastahiki au ni lazima awe na kofia ngumu. Pia nitoe wito kwa wananchi kuwaelekeza kwamba mtu yeyote au mwananchi yeyote asikubali kupakiwa katika chombo cha miguu miwili ambacho kinaendeshwa barabarani bila ya kuvaa kofia ngumu kwa usalama wao na maisha yao.

Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, kama nilivyoeleza bodaboda wote wamesajiliwa au vyombo vya moto vyote vimesajiliwa. Huu usajili ambao unaendelea ni kwa kuwawezesha kiuchumi wafanyabiashara hao ili biashara zao au kazi zao ziweze kukua na kuhakikisha kwamba hawana wasiwasi na maisha na Mheshimiwa Rais, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya hivi kuhakikisha kwamba wananchi wake wote basi wanakuwa na maisha ambayo hayana matatizo wala changamoto yoyote. Ahsante. (Makofi)