Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 25 Community Development, Gender and Children Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum 328 2025-05-15

Name

Asha Abdullah Juma

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ASHA ABDULLAH JUMA aliuliza: -
Je, ni lini Serikali itaanzisha utaratibu wa kuwasajili waendesha bodaboda nchini?

Name

Mwanaidi Ali Khamis

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WANAWAKE NA MAKUNDI MAALUM alijibu: -

Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Serikali inao mkakati wa kuwatambua na kuwasajili wafanyabiashara ndogondogo nchini wakiwemo waendesha bodaboda ambapo hadi kufikia tarehe 11 Mei, 2025 waendesha pikipiki (bodaboda) 3,032, Mwanaume 2,921 na Wanawake 111, walikuwa wamesajiliwa kwenye mfumo wa utambuzi, usajili na utoaji wa vitambulisho vya kidijitali.

Mheshimiwa Spika, usajili huo ni wa hiari na umeanza Machi, 2024 na unatekelezwa kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, TAMISEMI kupitia Dawati la Uratibu Wafanyabiashara Ndogondogo ambalo limeanzishwa katika Mamlaka za Serikali za Mitaa zote 184 nchini. Hivyo, zoezi la usajili linaendelea kwa kushirikiana na Maafisa waliopata mafunzo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini. Ahsante.