Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Margaret Simwanza Sitta

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Urambo

Primary Question

MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza: - Je, lini Uwanja wa Ndege Urambo utawekwa uzio ili kuimarisha usalama?

Supplementary Question 1

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Wizara, ninaipongeza kwa kufanya usafi katika Uwanja wa Urambo, ambapo sasa Uwanja unapendeza kwa kuwa upo katikati ya Mji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nina maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo:

Swali la kwanza, kwa kuwa uwanja huo upo katikati ya mji. Je, Serikali haioni kwamba kuna umuhimu wa kuweka utaratibu maalum wa kudumu wa usafi ili tusiwe tunangojea mpaka hali iwe mbaya ndiyo tuombe? (Makofi)

Swali la pili, kwa kuwa uwanja upo katikati ya Mji kwa ajili ya usalama na kupendezesha Mji pia. Je, Serikali haioni kuna umuhimu wa kuweka taa angalau za solar katika uwanja huo wa ndege? (Makofi)

Name

David Mwakiposa Kihenzile

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Mufindi Kusini

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, kwanza, kwa niaba ya Serikali kupitia Waziri wetu Mheshimiwa Prof. Mbarawa, tunapokea shukurani zake kwa sababu wachache ambao wakitendewa wema huwa wanashukuru. Wiki mbili zilizopita Mheshimiwa Sitta, alisimama hapa na akatoa ushauri wake na Serikali ikachukua jambo lake kwa uzito unaostahili, ikatekeleza. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pili, nimpongeze kwa jinsi ambavyo amekuwa mfuatiliaji makini wa maendeleo kwenye eneo lake. Amekuwa ni mmoja wa Wabunge wa kuigwa ambaye kila wakati anafuatilia maendeleo ya eneo lake. Ameleta maswali mawili la pili ni kama ushauri.

Swali lake la kwanza, nimhakikishie sisi kama Serikali tunajipanga kufanya jambo alilolieleza la usafi kuwa endelevu. Kwa hiyo, kila wakati tutajitahidi kuhakikisha kwamba usafi unafanyika katika Kiwanja hiki cha Ndege cha Urambo. (Makofi)

Swali lake la pili, Mheshimiwa Mbunge anaulizia kuhusiana na taa. Nimhakikishie kwamba Serikali imelipokea jambo hili kama ushauri, ninailekeza Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini iende kwenye eneo hilo ikatazame gharama zilizopo na kisha tutazame tunachoweza kukifanya ili kama alivyosema moja tuimalize ulinzi na usalama lakini pili tupendezeshe Mji wake wa Urambo, lakini tatu tuweze kuondoa vibaka pengine na wavamizi katika eneo hilo ambao wangeweza kuwa changamoto katika uendeshaji wa shughuli za wananchi za kila siku. (Makofi)

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Primary Question

MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza: - Je, lini Uwanja wa Ndege Urambo utawekwa uzio ili kuimarisha usalama?

Supplementary Question 2

MHE. BONIPHACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru. Tumekuwa na ahadi ya muda mrefu sana ya Uwanja wa Ndege wa Musoma, na sasa tumeambiwa kwamba miezi michache iliyopita kwamba utamalizika.

Je, ni lini uwanja huo sasa utamalizika ili wananchi wa Musoma wapate haki ya kupanda ndege?

Name

Boniphace Mwita Getere

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Bunda

Answer

NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI: Mheshimiwa Spika, ninampongeza Mheshimiwa Getere kwa kuuliza swali katika wa Uwanja wa Musoma ambao kimsingi wote tunafahamu, kihistoria huo ni Mkoa ambao Baba wa Taifa alikuwa anatokea ni Mkoa wenye madini, ni Mkoa wenye utalii.

Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kutambua uzito na umuhimu wa uwanja huu ulikwishafanya uamuzi wa kutenga fedha na ujenzi ulishaanza na hivi ninavyozungumza tupo asilimia 58.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge pamoja na Wabunge wetu wa Mkoa wa Mara kwamba tunaendelea na taratibu za ndani mara tu tutakapokamilisha taratibu za kifedha tutaukamilisha uwanja huo ili uanze kutumika na wananchi kwa sababu imekuwa ni kilio cha muda mrefu.