Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Daniel Awack Tlemai

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Karatu

Primary Question

MHE. DANIEL A. TLEMAI aliuliza: - Je, lini Serikali itatimiza ahadi yake ya kupeleka Shilingi Bilioni 4.5 Karatu ili wananchi wapate huduma ya uhakika ya maji?

Supplementary Question 1

MHE. DANIEL A. TLEMAI: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu ya maswali ya Serikali, nina swali moja la nyongeza.

Je, kwa kuwa ahadi imechukua miaka miwili toka Serikali itoe ahadi, nini mkakati wa Serikali ili kupunguza adha ya upungufu wa maji katika Mji wa Karatu? (Makofi)

Name

Maryprisca Winfred Mahundi

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI K.n.y WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, mkakati wa Serikali kuhakikisha Mji wa Karatu unapunguza kadhia ya maji, kwanza mradi huu ambao tayari tumeweka fedha zaidi ya Shilingi Bilioni 1.3 mwaka huu wa fedha 2025/2026 Wizara imetenga Shilingi Milioni 864 kuhakikisha kazi zitaendelea na kadri fedha zinavyopatikana basi tutahakikisha mradi huu unawekewa fedha ili uweze kukamilika.

Mheshimiwa Spika, sambamba na hilo Serikali itaendelea kuboresha mambo mbalimbali kama uchimbaji wa kisima ambacho kitakuwa zaidi ya mita 200, lengo ni kuhakikisha tunaweza kupata vyanzo vingine vya maji na kuweza kusambaza. Vilevile, visima ambavyo tayari vilichimbwa Wizara itahakikisha inakwenda kuviendeleza kwa kuhakikisha sasa vinasambaza katika maeneo yote yaliyokusudiwa. (Makofi)