Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 25 Water and Irrigation Wizara ya Maji 326 2025-05-15

Name

Daniel Awack Tlemai

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Karatu

Primary Question

MHE. DANIEL A. TLEMAI aliuliza: -

Je, lini Serikali itatimiza ahadi yake ya kupeleka Shilingi Bilioni 4.5 Karatu ili wananchi wapate huduma ya uhakika ya maji?

Name

Jumaa Hamidu Aweso

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Pangani

Answer

NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO NA TEKNOLOJIA YA HABARI K.n.y WAZIRI WA MAJI alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya kutekeleza miradi mbalimbali ya maji inayolenga kuboresha huduma ya majisafi na salama kwa wananchi wa Karatu Mjini. Katika mwaka wa fedha 2024/2025, jumla ya shilingi 1,371,878.043 zimetolewa kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Karatu (KARUWASA) ikiwa ni sehemu ya ahadi ya Serikali ya kuboresha huduma ya maji katika eneo hilo.

Mheshimiwa Spika, fedha hizo zimewezesha kukamilisha utekelezaji wa Mradi wa Maji Ayalabe na kuanza kwa utekelezaji wa Mradi wa Maji Bwawani Na. 3 ambayo kwa pamoja inanufaisha zaidi ya watu 18,880 kwa maeneo hayo.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutoa kipaumbele cha kupeleka fedha za utekelezaji wa miradi ya maji katika Jimbo la Karatu kadri fedha zinavyopatikana.