Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Supplementary Questions

Name

Zuberi Mohamedi Kuchauka

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Liwale

Primary Question

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA K.n.y MHE. DOROTHY G. KILAVE aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuongeza majengo katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke?

Supplementary Question 1

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Ninashukuru kwa majibu mazuri yanayotia matumaini kutoka Serikalini lakini nina maswali mawili ya nyongeza.

Mheshimiwa Spika, sambamba na ujenzi huo, bado Temeke kuna changamoto ya watumishi hasa wa Madaktari Bingwa. Je, Serikali ipo tayari inapofanya tathmini ya ujenzi huo iende sambamba na kuongeza watumishi kwenye hospitali hiyo? (Makofi)

Swali la pili, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Lindi ni hospitali chakavu, ni hospitali ya siku nyingi sana. Je, Serikali ipo tayari kuifanyia ukarabati hospitali hiyo ili iendane na wakati uliopo? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, ninaomba nijibu maswali mawili ya Kaka yangu Mheshimiwa Kuchauka, kama ifuatavyo:

Mheshimiwa Spika, moja ni kweli kwamba kuna baadhi ya maeneo kuna upungufu wa Madaktari Bingwa lakini ninataka nimhakikishie Mheshimiwa Kuchauka, katika hospitali zenye Madaktari Bingwa wengi moja wapo ni Temeke, lakini ni kweli tunapoongeza hili jengo na kwa sababu ya idadi ya watu tupo tayari pia kuongeza Madaktari Bingwa ili kukabiliana na namba ya watu itakayokuwepo kwenye eneo lile.

Mheshimiwa Spika, swali lako la pili, kuhusu Hospitali ya Mkoa wa Lindi, hii ni mojawapo ya hospitali za Mikoa ambazo huu upembuzi yakinifu na michoro inatengenezwa kwa ajili ya kuhakikisha inakuwa nayo mpya na kufanana na hospitali zingine za Mikoa. (Makofi)

Name

Aysharose Ndogholi Mattembe

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA K.n.y MHE. DOROTHY G. KILAVE aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuongeza majengo katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke?

Supplementary Question 2

MHE. AYSHAROSE N. MATTEMBE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Kwa kuwa, ujenzi wa Jengo la Covid-19 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida umekuwa ukisuasua.

Je, ni upi mkakati wa Serikali wa kupeleka fedha za kutosha ili kumalizia ujenzi wa jengo hilo?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, nimhakikishie tu Mbunge kwamba jengo hilo ni kweli kumekuwepo na tatizo analolisema na tayari mambo yameshafanyika Wizarani ya kuweza kulirekebisha hilo tatizo na nimhakikishie kabla ya Disemba jengo hilo litakuwa limemalizika. (Makofi)

Name

Oliver Daniel Semuguruka

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA K.n.y MHE. DOROTHY G. KILAVE aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuongeza majengo katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke?

Supplementary Question 3

MHE. OLIVER D. SEMUGURUKA: Mheshimiwa Spika, Hospitali yetu ya Rufaa ya Mkoa wa Kagera majengo mengi yamechakaa sana hasa OPD na wodi. Ningependa kuja Serikali ni lini itafanya ukarabati majengo hayo? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, ni kweli kama anavyosema Mheshimiwa Mbunge kwamba hospitali yao ni ya zamani na majengo mengi ni ya zamani, mengine yamefanyiwa ukarabati lakini bado ni yale ya zamani. Kwa hiyo, hii ni hospitali mojawapo ambayo michoro yake inachorwa kwa ajili ya kuja sasa na mkakati wa kuijenga upya na kubomoa yale majengo ya chini na kujenga majengo ya kwenda juu. (Makofi)

Name

Martha Festo Mariki

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA K.n.y MHE. DOROTHY G. KILAVE aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuongeza majengo katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke?

Supplementary Question 4

MHE. MARTHA F. MARIKI: Mheshimiwa Spika, Je, ni lini Serikali itatenga fedha kwa ajili ya umaliziaji wa Jengo la Mama na Mtoto katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Katavi? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, Hospitali ya Mkoa wa Katavi ni mojawapo ya hospitali nzuri sana na mpya ambazo Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Samia Suluhu Hassan amezijenga na amezindua hivi karibuni, lakini ni kweli kama anavyosema kuna jengo ambalo halijamaliziwa kama ambavyo amesema.

Mheshimiwa Spika, nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwenye bajeti ya mwaka huu fedha zinatengwa kwa ajili ya kumalizia kazi iliyopo pale. (Makofi)

Name

Abdallah Dadi Chikota

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nanyamba

Primary Question

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA K.n.y MHE. DOROTHY G. KILAVE aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuongeza majengo katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke?

Supplementary Question 5

MHE. ABDALLAH D. CHIKOTA: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa wodi nyingi za Hospitali ya Rufaa ya Ligula, Mkoani Mtwara zimechakaa.

Je, Serikali ina mpango gani wa kukarabati wodi hizo? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, Mtwara ni mojawapo ya eneo ambalo limepata bahati sana katika kazi ambazo zimefanywa na Rais wetu, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa sababu kilometa tatu tu kutoka hospitali hiyo ya Mkoa imejengwa hospitali nzuri sana ya Kanda ya Kusini.

Mheshimiwa Spika, pia ni kweli kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge anasema hospitali yao ni ya zamani imechakaa sana na ni mojawapo kama ambavyo nimesema kwenye hospitali zetu zote za zamani ni mojawapo ya hospitali ambazo michoro inatengenezwa kwa ajili ya kuja na mkakati baada ya kumaliza hospitali za Mikoa ambayo ilikuwa haina hospitali kabisa.

Name

Dr. Oscar Ishengoma Kikoyo

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Muleba kusini

Primary Question

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA K.n.y MHE. DOROTHY G. KILAVE aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuongeza majengo katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke?

Supplementary Question 6

MHE. DKT. OSCAR I. KIKOYO: Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya cha Kimea, Wilaya ya Muleba kilijengwa majengo mawili ya wodi za mama na mtoto kipindi kirefu hayakumalizika.

Je, ni lini Serikali itakamilisha ukarabati wa hayo majengo mawili?

Name

Dr. Festo John Dugange

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Wanging'ombe

Answer

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, nipo.

SPIKA: Haya, Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, majibu kwa Mheshimiwa Mbunge.

NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, ahsante. Ninaomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Muleba kwamba, tunafahamu walishaleta orodha ya vituo vya afya viwili ambavyo Serikali ya Awamu ya Sita ilishapeleka fedha kwa ajili ya ujenzi wa majengo lakini hayajakamilika, ninamhakikishia kwamba Serikali itapeleka fedha kwa ajili ya kukamilisha majengo haya ya vituo vya afya. Ahsante. (Makofi)

Name

Kilumbe Shabani Ng'enda

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Kigoma Mjini

Primary Question

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA K.n.y MHE. DOROTHY G. KILAVE aliuliza: - Je, kuna mpango gani wa kuongeza majengo katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke?

Supplementary Question 7

MHE. KILUMBE S. NG'ENDA: Mheshimiwa Spika, Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Kigoma, Hospitali ya Maweni mpaka sasa imechukua muda mrefu kukamilisha jengo la utawala.

Je, ni lini Serikali itakamilisha jengo la utawala la hospitali hiyo? (Makofi)

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA: Mheshimiwa Spika, kwanza niseme tu, Hospitali ya Mkoa wa Kigoma ni kweli ilikuwa na hali mbaya ya majengo kwa sababu ni hospitali ya zamani lakini kama Mheshimiwa Mbunge anavyokumbuka, hospitali hii ni mowapo ya hospitali alizozitembelea Mheshimiwa Rais kuzindua majengo mazuri sana yaliyojengwa kwenye eneo hilo. Kwa hiyo, ukiilinganisha Hospitali ya Mkoa ya Maweni iliyokuwepo na ya sasa kwa kweli hospitali hiyo imekuwa nzuri sana, na ni moja wapo ya hospitali zinazofanya vizuri sana nchini ipo kwenye top three ya hospitali zinazofanya vizuri kwenye nchi yetu.
Mheshimiwa Spika, ninamhakikishia Mheshimiwa Mbunge kuwa katika bajeti ya mwaka huu kwa kazi inayoijua inayoendelea pale nayo inatengewa fedha kwa ajili ya kumaliza kazi hiyo.