Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
2020-2025 Session 19 Sitting 25 Health and Social Welfare Wizara ya Afya 325 2025-05-15

Name

Dorothy George Kilave

Sex

Female

Party

CCM

Constituent

Temeke

Primary Question

MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA K.n.y MHE. DOROTHY G. KILAVE aliuliza: -

Je, kuna mpango gani wa kuongeza majengo katika Hospitali ya Rufaa ya Temeke?

Name

Dr. Godwin Oloyce Mollel

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Siha

Answer

NAIBU WAZIRI WA AFYA alijibu: -

Mheshimiwa Spika, Wizara inaendelea na maboresho ya miundombinu ya Hospitali za Rufaa za Mikoa Nchini ambapo kwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Temeke, Wizara inaendelea na maandalizi ya michoro ya usanifu kwa ajili ya ujenzi wa jengo la Huduma za Kliniki za Kibingwa na Bima. Utekelezaji wa ujenzi wa jengo hilo unatarajiwa kuanza katika mwaka 2025/2026.