Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Conchesta Leonce Rwamlaza
Sex
Female
Party
CHADEMA
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA K.n.y. MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza: - Je, lini ujenzi wa Bwawa la Yongoma - Same utaanza baada ya kukamilika kwa usanifu wa kina?
Supplementary Question 1
MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana. Kwa kuwa kata alizozitaja ambazo ni Maore, Ndungu, Kalemawe, Kihurio na Bendera, zimeathiriwa sana na ukame kutokana na hali ya mabadiliko ya tabia ya nchi na kwa kuwa wananchi wanashughulika na Kilimo. Je mnamkakati wa kumaliza bwawa hilo haraka ili wananchi waweze kufaidika? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, kuna mradi wa BBT katika Wilaya ya Muleba, Kata ya Kamachumu, Kata ya Ruhanga, Kijiji Makongola na mradi huo wananchi wanapanda …. na unaendelea vizuri lakini kuna tatizo kubwa sana la maji ya kumwagilia. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba maji yanapatikana ili mradi huu uweze kuwa na tija. (Makofi)
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kuhusu mpango wa kumaliza mradi huu wa Yongoma kwa haraka? Ndiyo, ni mpango wa Serikali na ndio maana tumeshakamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina na tumeweka kwenye bajeti ya mwaka 2025/2026 kwa ajili ya utekelezaji wa bwawa na eneo linalofaa kwa Kilimo.
Mheshimiwa Spika, ni ukweli ukanda ule wakati wa kiangazi, wakati wa masika wanapata maji mengi sana kwa muda mfupi, wakati wa kiangazi wanakuwa na ukame. Kwa hiyo, niwahakikishie tu wananchi wa maeneo hayo kwamba Serikali itaanza kujenga bwawa hili katika Mwaka wa Fedha wa 2025/2026 pamoja na eneo la hekta zaidi ya 1,000 ambazo zitakuwa ni kwa ajili ya Kilimo.
Mheshimiwa Spika, kuhusu mradi wa BBT wa Kagera, kwanza niseme tu niwakupongeze viongozi wa Serikali wa mkoa lakini nitumie nafasi hii kuwahakikishia na wewe mwenyewe Mheshimiwa Mbunge nikushukuru kwa wewe kuwa sehemu ya wakulima wa eneo lile, nakushukuru sana.
Mheshimiwa Spika, nikuhakikishieni tatizo la barabara zile kilometa chache tunaziweka kwenye bajeti ya mwaka kesho na tutawachimbia visima, kwa sababu tayari usanifu umeonyesha kwamba upatikanaji wa maji yapo, tutaleta magari kwa ajili ya uchimbaji kwenye eneo lile. (Makofi)
Name
Anne Kilango Malecela
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Same Mashariki
Primary Question
MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA K.n.y. MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza: - Je, lini ujenzi wa Bwawa la Yongoma - Same utaanza baada ya kukamilika kwa usanifu wa kina?
Supplementary Question 2
MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kupata nafasi hii, naomba kuuliza swali langu la nyongeza ambalo Mheshimiwa Waziri ni la muhimu sana. Kwa kuwa Bwawa la Yongoma linahitajika sana kwenye kata zilizotajwa hapo. Je, Serikali hamuoni kwamba mchukue ujenzi wa bwawa hili kama mkakati mkubwa wa Serikali? Ahsante. (Makofi)
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mama Kilango, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, yeye mwenyewe alinipeleka tukatembelea Ndungu, tukatembelea hadi kule juu milimani na ameona Serikali imeanza kutekeleza mradi wa Mlimani, tumeanza kutekeleza mradi wa skimu ya Ndungu. Nikuhakikishie Mheshimiwa Mama Kilango na wananchi wa Same, kama tulivyowaahidi kwenye mkutano pale kijijini mimi na wewe, mradi huu tutautekeleza na tutajenga bwawa hili na skimu hii kama inavyotarajiwa. (Makofi)
Name
Jackson Gedion Kiswaga
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Kalenga
Primary Question
MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA K.n.y. MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza: - Je, lini ujenzi wa Bwawa la Yongoma - Same utaanza baada ya kukamilika kwa usanifu wa kina?
Supplementary Question 3
MHE. JACKSON G. KISWAGA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naomba kuuliza swali. Je, ni lini sasa Serikali itakamilisha usanifu wa kina katika Bwawa la Magubike katika Kata ya Nzihi?
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kiswaga, kama ifuatavyo; -
Mheshimiwa Spika, wataalam wapo hatua za mwisho kumalizia Bwawa la Magubike na nikuahidi Mheshimiwa Kiswaga, kwenye bajeti ya mwaka kesho 2025/2026 Magubike itakuwepo na tutaanza ujenzi.
Name
Venant Daud Protas
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Igalula
Primary Question
MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA K.n.y. MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza: - Je, lini ujenzi wa Bwawa la Yongoma - Same utaanza baada ya kukamilika kwa usanifu wa kina?
Supplementary Question 4
MHE. VENANT D. PROTAS: Mheshimiwa Spika, ahsante. Bwawa la Goeko awamu ya kwanza lipo asilimia 98, tuna awamu ya pili na Mkandarasi ameshapatikana. Ni lini sasa Mkandarasi atakwenda kukabidhiwa site na kuanza ujenzi wa Bwawa la Goeko ambalo katika historia ni bwawa kubwa? (Makofi)
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Venant, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kwanza nimshukuru kwa support anayotoa kwenye mradi wa Goeko kama Mbunge, Mkandarasi ameshapatikana, mkataba umeshasainiwa na sasa tumepeleka maombi Wizara ya Fedha kwa ajili ya kupata advance payment kwa ajili ya yeye kwenda site. Nimuhakikishie tu kwamba mradi ule phase two unahusisha bwawa hilo kulikamilisha na vilevile kujenga jumla ya hekta 3,000 ambazo tulitembelea pamoja mimi na yeye kukagua lile eneo. Nashukuru.
Name
Dr. Christine Gabriel Ishengoma
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA K.n.y. MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza: - Je, lini ujenzi wa Bwawa la Yongoma - Same utaanza baada ya kukamilika kwa usanifu wa kina?
Supplementary Question 5
MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipatia swali la nyongeza. Ningependa kujua ujenzi wa Bwawa la Kidete utakamilika lini, ili kupunguza maporomoko ya Mto Mkondoa Wilayani Kilosa? Ahsante sana.
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, naomba tu nimwambie Mheshimiwa Ishengoma, kwamba Bwawa la Kidete ni moja ya mabwawa muhimu, kwa maana ya ukanda wa yale mabwawa matano yote, kwa ajili ya kuondoa matatizo ya mafuriko katika Wilaya ya Kilosa na Serikali itaendelea kusukuma kuhakikisha hiyo miradi yote inakamilika kwa wakati.