Jamhuri ya Muungano ya Tanzania

Primary Question

Term Session Sitting Sector Ministry Qn No Date
1961-1995 Session 1 Sitting 1 Livestock , Fisheries, Agriculture, Food Security and Cooperatives Wizara ya Kilimo 324 2025-05-15

Name

Naghenjwa Livingstone Kaboyoka

Sex

Female

Party

CHADEMA

Constituent

Special Seats

Primary Question

MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA K.n.y. MHE. NAGHENJWA L. KABOYOKA aliuliza: -

Je, lini ujenzi wa Bwawa la Yongoma - Same utaanza baada ya kukamilika kwa usanifu wa kina?

Name

Hussein Mohamed Bashe

Sex

Male

Party

CCM

Constituent

Nzega Mjini

Answer

WAZIRI WA KILIMO alijibu: -

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Kaboyoka, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo: -

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Kilimo kupitia Tume ya Taifa ya Umwagiliaji ilikamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Bwawa la Yongoma lenye ukubwa wa mita za ujazo 5.8 katika mwaka 2023/2024. Baada ya usanifu kukamilika, mradi huo umewekwa kwenye mpango wa ujenzi kwa mwaka 2025/2026. Kukamilika kwa ujenzi wa bwawa hilo kutawezesha kumwagilia eneo lenye ukubwa wa hekta 1,800 na kunufaisha wakulima 11,150 katika kata za Fidia, Ndungu, Kalemawe na Bendera.