Bunge la Tanzania
Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
Name
Mwanaisha Ng'anzi Ulenge
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE aliuliza: - Je, upi mkakati wa kuwaandaa Wanawake wakulima wa mbogamboga Mkoani Tanga kwenye mpango wa Tanga kuwa hub ya kilimo cha mbogamboga?
Supplementary Question 1
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa majibu mazuri ya Serikali, naomba kuuliza maswali mawili ya nyongeza kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Serikali imechagua Mkoa wa Tanga kuwa miongoni mwa kanda zitakazozalisha hot culture, hamuoni haja sasa yakutengeneza fikra za vifungashio, kumlinda mlaji na kuongeza thamani za mbogamboga zinazolimwa na wanawake wa Mkoa wa Tanga? (Makofi)
Mheshimiwa Spika, swali langu la pili, kwa kuwa sasa tumeona magari ya kuchimba visima vya umwagiliaji vimeshaingia nchini. Je, Serikali hamuoni haja ya kutoa kipaumbele kwa Mkoa wa Tanga kuchimbiwa umwagiliaji ili zile mboga kwa sababu ni mazao ya haraka yalete tija. Ahsante. (Makofi)
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Eng. Ulenge, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, mpango wa Serikali sasa hivi na Mkoa wa Tanga ni mmoja wa mpango huo, wataalamu wa wizara wameshaanza kufanya tathimini ndani ya Mkoa wa Tanga kwa mazao yote, kwa maana ya viungo, matunda na mbogamboga ili kuanzisha mfumo wa ukusanyaji wa mazao na namna ya kuyauza na kuyafungasha.
Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, ni mchakato ambao tunaendelea nao, na feasibility study inaendelea katika maeneo yote ambayo ni maeneo yaliyoteuliwa kama maeneo ya uzalishaji wa mbogamboga na viungo. Kwa hiyo, nataka nimtoe hofu na niwaambie wananchi wa Mkoa wa Tanga kwamba ni jambo ambalo Serikali inalifanyia kazi na hivi karibuni tutakuwa na taarifa rasmi kwa ajili ya kuanza kutekeleza.
Mheshimiwa Spika, kuhusu uchimbaji wa visima, nataka niseme tu kwa Wabunge wote, mikoa yote itapewa kipaumbele. Lakini tutawapa vipaumbele maeneo ambayo tayari tathimini ya awali imeshafanyika, mpaka sasa tathimini ya awali imeshafanyika kwa halmashauri 75 ambazo zitaanza kufanyiwa huu utaratibu na utaratibu wa uchimbaji wa visima hivi, hivi karibuni Serikali itautangaza kwa kuwa na mwongozo, tutakuwa na skimu ya wakulima watako chimbiwa bure kwa 100% lakini watakuwepo wakulima ambao watakuwa wanachangia gharama kidogo ili waweze kuchimbiwa.
Mheshimiwa Spika, mfumo wa uchimbaji hautakuwa kila mkoa kupelekewa gari, Serikali imenunua magari zaidi ya 22, 23 ambayo mpaka tarehe 15 Juni, yatakuwa yamefika yote, then tutatangaza ni mkoa gani tunaanza kuchimba. Kwa hiyo, niwaombe Waheshimiwa Wabunge, tusubiri baada ya hiyo public announcement itakayofanyika kila mkoa utafahamu magari yatakwenda lini katika mkoa husika.
Name
Dr. Thea Medard Ntara
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Special Seats
Primary Question
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE aliuliza: - Je, upi mkakati wa kuwaandaa Wanawake wakulima wa mbogamboga Mkoani Tanga kwenye mpango wa Tanga kuwa hub ya kilimo cha mbogamboga?
Supplementary Question 2
MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Je, Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba zile mbegu zinazouzwa madukani zote zina ubora na zina bei nafuu ili wanawake waweze kuzinunua kwa uhakika?
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ntara, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, suala la ubora Serikali imeendelea kuongeza uwezo wa taasisi yetu ya udhibiti ya Mbegu ya TOSCI na msimu ujao wa Kilimo Wakulima wataona kuna new label ambayo inawekwa katika mifuko yote iliyopo sokoni, hilo la kwanza.
Mheshimiwa Spika, la pili, ili kutatua tatizo la mbegu fake, Serikali imeamua sasa hivi kusajili upya wauzaji wa vijijini, wa mikoani na kuubadili mfumo wa usambazaji na wasambazaji wote wataingizwa kwenye database maalum.
Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la kupunguza gharama, Serikali imeanza kuweka ruzuku katika mbegu; tumeanza Ngano, Alizeti na sasa tumeingiza zao la Mahindi. Malengo ya Serikali ni kuhakikisha kwamba tunapunguza gharama za Mbegu kwa wakulima.
Mheshimiwa Spika, lakini vilevile tumeanza kuihusisha sekta binafsi kuanza kutumia mashamba ya Serikali ambayo yalikuwa hayatumiki kabisa yamegeuka mapori kwa ajili ya kuongeza uzalishaji wetu wa mbegu ili kuweza kuhakikisha kwamba availability na affordability inatokea sokoni. Ahsante. (Makofi)
Name
Dr. Angeline Sylvester Lubala Mabula
Sex
Female
Party
CCM
Constituent
Ilemela
Primary Question
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE aliuliza: - Je, upi mkakati wa kuwaandaa Wanawake wakulima wa mbogamboga Mkoani Tanga kwenye mpango wa Tanga kuwa hub ya kilimo cha mbogamboga?
Supplementary Question 3
MHE. DKT. ANGELINE S. L. MABULA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Manispaa ya Ilemela inao Wakulima wachache wanaolima mbogamboga kutokana na eneo kuwa dogo. Je, Serikali haioni sasa ili kuongeza tija kwa wakulima wale kuwaanzishia vitalu nyumba ili waweze kuzalisha mazao kwa tija?
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mabula, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, kwanza nikiri ameshakuja ofisini kwangu, tumeshakaa na nataka nimuhakikishie yeye na wakulima wadogo wa Wilaya ya Ilemela, Serikali inaanza kulifanyia kazi baada ya bajeti ya mwaka huu, skimu ya Wakulima wa Ilemela na maeneo hayo; Lake Victoria yote wataona ndani ya bajeti ya Serikali tumeweka mpango kwa ajili yao. (Makofi)
Name
Saashisha Elinikyo Mafuwe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Hai
Primary Question
MHE. ENG. MWANAISHA N. ULENGE aliuliza: - Je, upi mkakati wa kuwaandaa Wanawake wakulima wa mbogamboga Mkoani Tanga kwenye mpango wa Tanga kuwa hub ya kilimo cha mbogamboga?
Supplementary Question 4
MHE. SAASHISHA E. MAFUWE: Mheshimiwa Spika, ahsante. Katika Jimbo la Hai, wapo wananchi wengi wanaolima zao la Nyanya kwa wingi na kufanya zao hili kuwa sokoni kwa wingi na bei yake kushuka.
Je, ili kudhibiti thamani ya zao hili la Nyanya, Serikali ina mpango gani wa kujenga kiwanda cha kuchakata zao la Nyanya katika Jimbo la Hai, ili thamani ya zao hili iweze kuongezeka? (Makofi)
Name
Hussein Mohamed Bashe
Sex
Male
Party
CCM
Constituent
Nzega Mjini
Answer
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, nataka nijibu swali la Mheshimiwa Saashisha...
SPIKA: Mheshimiwa Waziri, majibu.
WAZIRI WA KILIMO: Mheshimiwa Spika, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Saashisha, kama ifuatavyo: -
Mheshimiwa Spika, naomba nisiseme sasa hivi tuna mpango kwa ajili ya Hai lakini nimelipokea, tunaweza kukaa pamoja kujadili, kuangalia scale kama ambavyo tumekaa pamoja ku-unlock matatizo ya masoko mawili katika jimbo lako kwa ajili ya Wakulima wa mbogamboga. Kwa hiyo, nikuombe tu kwamba mimi na wewe tupate muda tuweze kujadili, tutatuma wataalamu tuangalie ili tuwe na mpango, kila eneo lina mpango wake.
Mheshimiwa Spika, lakini kuhusu kuongeza thamani nataka niwahakikishie Wabunge, kwenye bajeti tutakayokuja nayo tutakuwa na mpango maalum wa uongezaji wa thamani ambao utasimamiwa na Wakulima wadogo (backyard processing) kwa mazao yote ili tuweze kuongeza thamani ya mazao yetu sasa hivi. (Makofi)